Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda.



TAREHE 3-4-2014
















MCHUMBA MTARAJIWA WA SAMATTA.





Takribani miaka minne iliyopita Mshambuliaji Nyota wa kimataifa toka Tanzania anayekiputa katika timu ya TP Mzembe, MBwana Aly Samatta alikuni ni mchezaji wa kawaida sana pale alipokuwa akiitumikia Timu ya African Lyon ya Mbagala Jijini Dar es sam.

Samatta  mwenye umri  miaka 22 kipaji chake kiliongezeka mara dufu baada ya kujiunga na wekundu wa msimbazi simba ambapo kwa kipindi hicho alikuwa akitumikIa mfurulizo katika timu ya Taifa ya Wakubwa pamoja na timu ya Vijana  na klabu yake ya Simba hali ambayo iliwashawishi TP Mazembe kuanza kumnyatia kimya kimya hasa alipowasumbua vilivyo katika mtanange ambao timu hizo zilikutana katika ligi ya Mabingwa afrika.

Uwezo wake wa uwanjani   umepokewa kwa vifijo na Ndelemo kwa Mashabiki wa Mjini Rubumbashi na wamempachika  jina la 'SAMA GOALS' baada ya kufumania nyavu mara 6 katika michuano ya CAF msimu uliopita na kufanikiwa kuzisumbua sana timu za Al Ahly,Zamarek,Berukum Chelsea,Pawor Dynamos pamoja  Al-Merrikh.

Kwa kulitambua hilo TP Mazembe  wameboresha maisha ya Samatta kimapato  ambapo inaelezwa kuwa Thamani ya Mbwana Samatta ni Dola za kimarekani 450,500 zaidi ya shiringi bilioni 1.2.

Toka alipotua inchini Congo Miaka Miwili iliyopita baadhi ya timu zingine kubwa zimekuwa zikimpigania ili kunasa saini yake,ikiwemo klabu ya Al Ain inayoshiriki katika ligi kuu ya Falme za kiarabu UAE ambayo ipo tayari kumlipa zaidi na kupandisha thamani yake ya hivi sasa ya dola 450,000 ,hata hivyo kwa sasa Mmiriki wa timu hiyo Moses Katumbi hawezi kumwachia mshambuliaji huyo tegemezi katika timu hiyo kwa sasa mara baada ya kumuuza Mputu kwa kuwa TP Mazembe ndoto yake ni kuchukua ubingwa wa Afrika pia ikibidi  ubingwa wa dunia kwa ngazi ya Vilabu ambapo Samatta ni mshambuliaji tegemeo kwa mabingwa hao wa kongo.

Mbwana Aly Samatta

kuzaliwa -1992

eneo  - Dar,Mbaga

Timu Alizochezea;-
2008-2010  African Lyon,

2010-2011  Simba,

2011-Mazembe.    

Chapisha Maoni