Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Ali Yusuph Maarufu kwa jina la Tigana ambaye alifanikiwa kutikisa soka la hapa nchini kwa kucheza simba na Yanga pia timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na timu za nje.
Ilipoishi jana………..
“sijisifii ila kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kusakata kandanda nimefanikiwa kutumukia kikosi cha timu ya taifa kwa misimu mingi sana,ambapo ifuatayo ni baadhi ya miaka ambayo naikumbuka nimechezea timu ya Taifa,mwaka,1993,1994,1996,1998,2001 pamoja na mwaka 2005 ambao ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kuitwa timu ta Taifa.
 Endelea………………
Tukio kali
Anacheka kisha anaendelea; ”katika mchezo wa soka kama timu yenu ikipata ushindi wachezaji ufarijika sana,sasa kilicochotokea  baada ya kumalizika kwa mchezo wetu mjini Bulawayo kati ya yanga na wapinzani wetu Said Maurid alinitonya kuwa kuna zawadi  ya mchezaji bora  twende tukachukue ambapo yeye alikuwa nyota wa mchezo ule na aliniambia kuwa zawadi hiyo ni boksi moja la castle leager.

“mimi nilifurahi sana na nikamwambia SMG asitoe taarifa kwa mtu mwingine adi baada ya kuchukua kile kinywaji,kweli tukaenda kwa uongozi wa siku ile na tukakabidhiwa mzigo wetu tukaondoka nao baada ya kuondoka Said Maurid yeye alikuwa hatumii pombe mimi nikachukua lile furushi nikaenda nalo chooni nikafungua haraka na kuitoa castle nne na nikafungua moja nikaaza kubugia huku nikipita kuimba huku nikiwatonya wenzangu kwa ishara kuwa waende chooni kuna mzigo.

“wachezaji wezangu wakaenda chooni kuvamia ule mzigo ambapo kuna wengine walichua mbili mbili wengine moja pi wapo ambao walikosa, sherehe ikaendelea  mpaka tulipokwea pipa kuelejea nyumbani Tanzania.

Tulisafiri kwa basi na timu ya Taifa adi Zambia.
“mwaka 2003 timu yetu ya Taifa la Tanzania sisi tukiwa wachezaji tulienda kwa usafiri wa Basi toka Dar es Salam adi Zambia isipokuwa wachezaji watatu ndio walienda kwa usafiri wa ndege akiwemo Juma Kaseja pamoja na Pawasa kiukweli tulichoka sana kwa kuwa tulikaa kwenye basi kwa muda mrefu Sana.
“siku ya mechi wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia walicheza mpira mzuri sana kushinda sisi kwa kuwa tulikuwa bado na uchovu wa safari ingawa juma kaseja alicheza vizuri sana siku ile hata hivyo zambi walitutungua bao nyingi na wao wakasonga mbele sisi Tukarudi nyumbi mikono kichwani.

Wachezaji  nyota.
“Tegete wa yanga alikuja vizuri sana lakini kwa sasa amejilemaza kiwango kimepungua pia mchezaji wa kimataifa wa Rwanga beki mbuyu Twete anafanya vizuri.

Ushauri.
“rais Malinzi ajitaidi kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kwanza nampongeza kwa mpango wake wa kuzunguka nchi zima kusaka vipaji kwa ajili ya timu imara ya Taifa,pia  wasimamie uwepo wa shule za michezo za ukweli ili kuakikisha soka letu linafika mbali kimataifa.


Maisha baada ya soka.
“Umri wangu ni miaka 43 nina cheti cha ukocha nafundisha timu ya Daraja la kwanza ya Frend Rangers ,pia nafanya biashara ndogo ndogo,na nina watoto watatu”,Anaitimisha Ali Yusuph Maarufu kwa jina la Tigana ambaye alifanikiwa kutikisa soka la hapa nchini kwa kucheza simba na Yanga pia timu ya Taifa ya Tanzania.
MWISHO,MWISHO.
ENDELEA KUFUATILIA JELAMBA VIWANJANI KWA MAKALA MBALI MBALI ZA WACHEZAJI WA ZAMANI.
  Line ni usafiri wa uhakika na salama usisumbuke kuuliza usafiri ...


Chapisha Maoni