Stivin Mapunda [GARRINCHA] aliyevaa Tsherti nyeusi kulia.
Stivini mapunda [Garrincha] ni
miongoni wa washambuliji hatari sana ambao wamewai tokea hapa nchini na
akafanikiwa kutikisa soka la Tanzania kuanzia mwaka 1997-2005,akichezea timu
ya Maji Maji ya Songea ,Wekundu wa Msimbazi ‘Simba’ na Timu ya Taifa
[99-2005]
Garrincha alianza kucheza soka toka
shule ya msingi Hanga, Darasa la tatu akiwa na miaka 9 na akiwa sekondari
alifanikiwa kushiriki michuano mbali mbali ya shule pamoja na Umiseta hadi
ngazi ya Taifa ambapo kipaji chake kikaonekana na kuanza kung’ara nchi zima.
katika kipindi hicho akiwa shule ya
msingi Garricha alipata nafasi ya kwenda kucheza soka Ulaya kupitia kwa mzungu
aliyekuwa kocha wa maji maji wakati huo ambaye alikiona kipaji chake wakati
timu hiyo ilikuwa ikiweka kambi mara kwa mara huko Hanga, lakini baba
yake alikataa kutokana na kuofia usalama wa mwanao kwa kuwa alitaka
mwanao asiende mbali nae:-anasimulia….
“Kocha wa maji maji kipindi hicho
toka Brugaria alitaka kunichukua ili nikasome ulaya Pamoja na kuendeleza kipaji
changu cha Soka baada ya kukiona kipaji changu shuleni Hanga wakati wao
walipokuwa wameweka kambi, bahati mbaya baba yangu alikataa kwa kuofia usalama
wangu pindi nitakapo kuwa mbali nae hivyo ikashindikana,alisema mapunda.
mwaka 1993 Mapunda alianza kucheza
soka la ushindani akiwa na timu ya Taiger mbeya timu ambayo alicheza kwa
kujituma sana ambapo kiwango chake kiliongezeka siku hadi siku na mwaka 1997
alitua rasmi katika Timu ya Maji maji maarufu kama wanalizombe toka mkoani
Ruvuma.
mapunda alicheza kwa umahili mkubwa
akiwa na maji maji ambapo aliiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa wa Tanzania
kwa mara ya Tatu mwaka 1998 katika ligi ya muungano na yeye alifunga magori
ambayo yaliiwezesha timu ya Maji majikuchukua kombe la ligi ya muungano kwa
mara ya tatu.
Garrincha anawataja baadhi ya
wachezaji wa kikosi cha wanalizombea ambao walichukua ubingwa mwaka 1998
ni pamoja na Ivo Mang’itu[marehemu],John Alex,Amri Said, Martin,Stivin
Mapunda,Twaa omari[marehemu],Godfrey kikumbizi,Kelvin haule,Said
msham[marehemu] pamoja na Omari Husein ambao waliipeleka Maji Maji kwenye
michuano ya kimataifa.
Hata hivyo kutokana nyota yake
kuendelea kung’ara kwa kiwango cha hali ya juu sana na kusakwa na timu kubwa
hapa nchini ilimlazimu kuipa kisogo timu yake ya nyumbani na
akajiunga na Wekundu wa msimbazi Simba,mwaka 1999,timu ambayo aliichezea kwa
mafanikio makubwa sana na aliisaidia timu hiyo kunyakua mataji mbali mbali
iiwemo kombe la Tasker,ligi kuu bara, pamoja na kombe la mapinduzi lakini kubwa
zaidi alisaidia kuifikisha Simba kwenye robo fainali ya clabu bingwa afrika
mara baada ya kuwasambalatisha vigogo wa soka toka Misri[ Zamareck] kwa
mikwaju ya Penalti na kufanikiwa kuingia Robo Fainali.
Safari yao katika ligi ya mabingwa
iliishia Robo fainali mara baada ya kuchezea kipigo toka kwa Mabingwa wa Ivory
[Isec Mimosas] katika mechi ya marudiano ambayo Simba walichezea Ugenini na
hatimaye wakaaga Rasmi mashindano..............................
usikose kufuatilia makala hii ya Stivin Mapunda ataendelea kusimulia mengi kuhusu historia yake ya soka ikiwemo Tukio la kufungiwa siku nne nchini Nigeria AKIWA NA TAIFA STAR.
Chapisha Maoni