Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



MICHUANO ya kumwenzi mwasisi wa Mpira wa miguu mkoani ruvuma dokta
Roulance Gama maarufu kama Gama Cup yamemalizika hivi karibuni mjini
songea, kwa timu ya Lizabon City kunyakua ubingwa baada ya  kupata
ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa fainal.

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na Mtoto wa Mzee Gama, Musa Magama
Mshindi wa kwanza amejipatia jenzi seti moja,kikombe pamoja na
shiringi laki moja na nusu mshindi wa pili aliondoka na ngao,mipira
miwili pamoja na shiringi laki moja huku mshindi wa tatu Holly Family
akiibuka na kitita cha shiringi elfu Hamsini vile vile mpira mmoja.

Msimamizi mkuu wa mashindano hayo God Mvula alisema mashindano hayo
yatakuwa endelevu kutokana na amasa kubwa ambayo imetokea toka kwa
wadau wa soka huku wadau wote wa mpira mkoani ruvuma wakiimba na
kutaja jina la Dokta Gama.

"kumwenzi Gama ni suala ambalo muhimu kwetu ili kupata baraka zake kwa
kulitambua hilo tumepanda kufanya mashindano hayo kila mwaka suala
ambalo wadau wengi wa michezo wamekubari kulitekeleza.

Chapisha Maoni