Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




“Dewji baada ya kutoka Uingereza alinitafuta sana ili kusaini mkataba Simba kwa kipindi hicho aliwatuma watu wake lakini nilikuwa nikiwapiga chenga kwa kuwa kipindi kile mawasiliano yalikuwa magumu nilifanikiwa kuwatoroka adi msimu uliponza nikavaa uzi wa Pan Afrika.

Songa nayo……………………………

Ushirikina.
“ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo kama timu zetu hazitaamua kuchana na Imani hizo hasa hapa nchini,baadhi ya timu zetu suala la kutumia madawa ya kienyeji siku za mechi ni ishu ya kawaida sana,Mimi binafsi siamini Imani hizo kwa kuwa mpira ni Mazoezi nchi zote ambazo nimeinda kusakata kandanda la kuripwa Imani hizo hakuna wao ni mazoezi pamoja na mbinu za kocha.

Mechi hii kiboko..
“moja ya mechi ambayo naikumbuka katika michezo yote ambayo nimewai cheza katika maisha yangu ya soka ni mchezo kati ya Yanga na Timu ya Bulawayo Ilenders ya nchini Zimbabwe katika klabu bingwa Afrika,mechi ya kwanza ilifanyika Jijini Dar esalam ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 2-2 matokeo ambayo yaliwakatisha tamaa viongozi wengi wa Yanga kwa kuwa ilitakiwa kwenda nyumbani kwao.

“safari ya kwenda katika mchezo wa Marudiano viongozi wengi wa yanga waligoma kwenda meneja pekee alikubari kusafiri na timu hadi Bulawayo,ambapo siku ya mechi mashabiki wa Ilenders walitupa presha sana  ambapo kila mmoja wao alikuwa ameshika bango ambalo lilisomeka 5-0 na uwanja wa Bulawyo ni mkubwa sana na siku hiyo ulitapika,basi mimi  kipindi cha kwanza nikawapiga bao,uwanja wote ulikuwa kimya hapo ndipo tukapata nafasi ya kucheza kwa Amani.



“kipindi cha pili Said maurid SMG aliwakimbiza na akawatundika bao la pili bao ambalo liliwachanganya sana mashabiki wao na ikaperekea wachezaji wao wacheze kwa presha kubwa,dakika za mwisho tulipata penalti ambayo ilizua vurugu kwa mashabiki adi ilipelekea mpira kumalizika bila sisi kupiga penalty ile,mashabiki walikuwa wakirusha chupa ngumu uwanjani kiasi kwamba ilikuwa kila tukisogea kupiga penalty walizidi kurusha chupa nyingi Zaidi ambapo mwamzi bada ya kuona hali tete Zaidi akamua kumaliza mpira.

“kingine ambacho kilitokea baada ya kumalizika ule mchezo mashabiki walituzuia kutoka uwanjani ilikuwa kila tukitoka wanarusha chupa na kitu ambacho tulikifanya tulichukua makoti yetu na kuweka kichwani huku tukitimua mbio kuelekea katika chumba cha kubadilishia nguo,nakumbuka siku ile tulipigwa sana chupa za mgongoni na mashabiki.

“baada ya mchezo huo nakumbuka tulipangiwa na Mamelodi sundowns toka nchini Afrika ya kusini ambapo katika mchezo huo mimi na Said mwamba tulifungiwa kwa madai ya utomvu wa nidhamu basi yanga ikapoteza mbele ya waafrika kusini na ikaaga mashingano.

Itaendelea kesho tarehe 25-04-2014 Ikiwemo kipa wa yanga doe mokey kususia mchezo kisa………… usikosi .


Chapisha Maoni