Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 TAREHE 10-04-2014

Robben
Matumaini ya timu ya Manchester United kufanya maajabu katika ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA yaliyeyuka jana usiku wa Jumatano baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich ya Ujerumani cha magoli 3-1.
Hayo yalikuwa ni matokeo ya mchezo wa marudiano baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford, timu hizo kutoka sare ya magoli 1-1.
Kikosi cha kocha David Moyes, kilionekana kingebadili matokeo hayo na kupenya hatua ya nusu fainali baada ya beki wa kushoto wa Manchester United Patrice Evra kuukwamisha mpira kimiani kufuatia kombora kali alilolimimina katika lango la Bayern na kuifanya timu yake iongoze katika dakika ya 57 ya mchezo.
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia goli

Hata hivyo furaha ya Manchester haikudumu kwani katika dakika ya 59 mshambuliaji wa Bayern, Mario Mandzukic aliisawazishia timu yake kwa mpira wa kichwa.
Vijana wa Bayern walizidisha mashambulio katika lango la Manchester United na juhudi zao zilizaa goli katika dakika ya 68 lililofungwa na Tomas Muller.
Arjen Robben alihitimisha safari ya Manchester United baada ya kukwamisha goli la tatu katika dakika ya 76 na kuifanya Bayern Munich kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.
UEFA inatarajia kupanga makundi mawili ya timu nne zilizofuzu kucheza hatua ya nusu fainali.
Timu hizo ni Bayern Munich mabingwa watetezi ya Ujerumani walioitoa Manchester United, Atletico Madrid ya Hispania ikiwaondoa Barcelona pia ya Hispania, Real Madrid nayo ikiindoa katika michuano hiyo Borrusia Dortmund ya Ujerumani na Chelsea ya Uingereza ikiisambaratisha PSG ya Ufaransa.

Chapisha Maoni