TAREHE 10-04-2014.
Na S ophia
Mwaipyana,Mbeya.
Ukiwazungumzia wanawake wapiganaji katika soka
nchini Tanzania basi huta sita kumtaja
Elizabeth Kalinga aliyejikita katika soka akiwa ndiye mwamuzi katika mpira wa miguu.
Elizabeth huyu ndiye mwamuzi wa kwanza mwanamke katika nchi yetu aliyefanya kazi
hii ya uamuzi kwa kipindi kirefu akiwa kama mwanamke, amejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa ni wanawake wachache wamefanikiwa kuhimili kufanya kazi katika sekta ya michezo.
Lakini kwa
mwanamke huyu aliye jaa ujasiri mkubwa
yeye hakuamini kauli iliyo kuwa
imetawala katika jamii nyingi za kitanzania ambayo ilimwona mwanamke
hawezi kitu na walikuwa wakibaguliwa sana katika sekta mbalimbali.
Mwanamke
huyu shujaa alijikita katika kazi ya uamuzi na alikubalika sana kwa utendaji
wake mzuri wa kazi yake japo wengi walimchukia kuona akiwazidi kiwango cha uamuzi
kwani mwanadada huyu alikuwa na uwezo mkubwa sana katika kazi hii ya uamuzi.
Ulianza lini kazi hii ya uamuzi?
Nilianza
kujifunza kazi hii ya uamuzi mwaka 1980 mafunzo hayo niliyachukulia nchini
Zambia na ndani ya mwaka huu nilianza kuchezesha ligi daraja la tatu.
“nilikuwa na
uwezo mkubwa sana wa kuchezesha soka hata kuwashinda wanaume ilifika kipindi
nilikuwa nikipangiwa kuchezesha mechi ngumu zote nilikuwa nikipangiwa mimi kwa
kujua kuwa ninauwezo mkubwa wa kuchezesha mchezo bila upendeleo”
Mechi gani
ilikuwa ngumu kwako?
“sikumbuki
mwaka lakini hii ndiyo ilikuwa mechi ngumu sana kwangu ilikuwa ni katika ya
timu ya Yanga na Mirambo siku zote timu ya Mirambo walikuwa wakorofi sana”
“lakini
kwangu walijikuta wakiwa wapole kutokana nilichezesha ile mechi bila upendeleo
palipo kuwa panastahiri kutoa adhabu nilitowa bila kujali huyu ni mchezaji wa timu gani”
Changamoto
gani ulizo kuwa ukikutana nazo katika kazi yako.
“kama unavyojuwa kipindi kile watu walikuwa wanamwona mwanamke hawezi kitu hivyo walikuwa
wana nidharau lakini nashukuru mungu walikuwa wananiheshimu”
“pia mechi
nyingi ngumu nilikuwa napewa nichezeshe mimi walikuwa wakihisi nitashindwa, kunawakati walifanya mambo kwa
kunikomoa kwani kuna baadhi ya makocha na viongozi walianza kunichukia baada ya
kuona nawazidi umahili kwani ilifika wakati jamii ilinikubali sana“
Vipi kuhusu
rushwa kwa waamuzi.
“kiukweli
vishawishi vipo lakini swala la kupokea au kukataa ni uamzi wa mtu na kumbuka kunamechi moja sikumbuki mwaka viongozi wa timu Fulani
walimpa msaidizi wangu rushwa aje anipe mimi”
“alipoleta
nilimwambia kaanazo mchezo ulipo malizika wale viongozi wakanifwata wakiniuliza kwanini tumekupa pesa halafu timu
yetu haujaifanyia msaada uwanjani nikawauliza
mlinikabidhi mimi hizo pesa?, kwahiyo vishawishi nivingi ila mwamuzi yeye mwenye
ndiye anatakiwa kuwa na msimamo”
kazi hii ina ugumu gani?.
“kazi hii
haina ugumu wowote ilimradi uzijuwe sheria na kufanya mazoezi kila wakati ila ukiwa
mvivu ndipo kazi hii huwa ngumu”
Nini
utofauti wa waamuzi wa sasa na zamani
“waamuzi wa zamani tulikuwa hatuwezeshwi, tunajitegemea vifaa vya michezo
pia tulikuwa tukipewa nauli peke ,lakini
waamuzi wa sasa wanawezeshwa”
“pia wamuzi
wa zamani walikuwa wakipewa kazi hii ikiwa unakazi nyingine walikuwa wakihofia
iwapo mtu akipewa hana kazi nyingine walihofia ata shawishika na kupokea
rushwa”
Tukio gani
ambalo huwa haulisahau
“kitu
ambacho huwa hakinitoki katika kumbukumbu zangu ni katika ya mwaka 2000 au 2001
nilipolipwa shilingi 5000 tu baada ya
kuchezesha mechi ya Mtibwa na Prison ambayo walichezea Morogoro”
“pesa hiyo
nilipewa ikiwa ni garama zote za mchezo hivi vilikuwa ni visa kwa viongozi ambao walitaka niipendele timu yao kwakuwa walikuwa
nyumbani,iliniadhimu nitumie pesa zangu mwenyewe kurudi nyumbani Mbeya”
Jamii
ilikuwa inakuchukuliaje
“kiukweli
kwa miaka ile watu wengi walikuwa wana niona kama muhuni flani na msichana wa
ajabu sana kulingana na utamaduni wetu wa kitanzania mtoto wa kike walikuwa wakimdharau sana”
Unalionaje
soka la mkoa wa Mbeya kwa sasa.
“katika
mikoa iliyo jaliwa Baraka ya vipaji vingi katika soka basi mbeya ni moja
wapo,soka linazidi kukuwa kwani mkoa sasa una timu mbili ligi kuu na moja ligi
daraja la kwanza hivyo maendeleo ni makubwa sana na wadau wazidi kuzisapoti timu
zote
Uashauri
wako kwa vijana pamoja na wachezaji
“wachezaji wajitume kwa bidii iliwajitangaze huku waki
zingatia nidhamu na mafunzo wanayo fundishwa na walimu wao iliwawezesha kuwa
wachezaji wa kimataifa”
“kwani
kupitia mpira tunapunguza tatizo la ajira kwa vijana na tunaweza kuondoa
umasikini kwani mpira nikazi kama kazi nyingine”
Katika
familia yenu nani amefuata nyayo zako?.
“hapana ila
alikuwepo mdogo wangu ambaye nilimfundisha ubondia lakini kwa bahati mbaya
alifariki,lakini yupo mjukuu wangu ambaye anapenda sana kazi kama yangu naimani Yule atarithi mikoba
yangu”
Baada ya
kuachana na soka mwaka 2002
Kwasasa ni mtendaji
wakata ya Ruanda na katibu tarafa wa kata hiyo ,lakini katika soka ni mwenyekiti wa soka la wanawake mkoa”
Soka la
wanawake katika mkoa wetu lipo vipi.
“kuna watoto
wenye vipaji vizuri hivyo wazazi na wadau wasoka tunawaomba wazidi kuwapa
sapoti watoto wakike kwani nao wana weza”
Chapisha Maoni