Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


JOHN KABISA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAJI MAJI ENDELEA KUFUATILIA STORI YAK,ANAITIMISHA
FC Leopald walitulinganisha na timu ya shule.

“Mwaka 1986 katika michuano ya Club Bingwa Afrika tulipambana na Fc Leopald ya Kenya ambapo wezetu wakenya walitudharau sana adi walidiliki kukifananisha kikosi chetu na timu ya shule na kuhaidi watatufunga zaidi ya bao 6,

“Nakumbua katika mchezo huo nilicheza vizuri sana na baada ya mechi niliandikwa sana na vyombo vya habari vya Kenya kutokana na shughuli ambayo niliwaonyesha siku ile ingawa wakenya walitufunga bao 1-0, na ilikuwa kinyume na matarajio yao.

“Na mchezo wa marudiano mchezo  ambao ulichezwa Mjini Arusha FC leopald walitubamiza tena bao 1-0 na wakafanikiwa kusonga mbele.

Waamzi

“Ni wavivu sana kubadilika,zamani waamzi walikuwa wanafanya vizuri licha ya techinologia kuwa chini,lakini siku izi wanaweza kujifunza toka nje kupitia Tv pamoja na mitandao.

Mchezaji anayemhusudu

“Mcheaji ambaye namkubari sana kwa hawa wanaocheza sasa hivi hapa Tanzania na anaitendea haki nafsi ya kiungo  ni mchezaji tegemeo wa Azam Fc Abul Bakari [Sure Boy] ,Mora amjali zaidi.

Timu ya Maji maji.

“Timu imepoteza mwelekeo kwa asilimia kubwa kutokana na kuyumba kiuchumi pamoja na kukuwa na viongozi wenye mtanzamo chanya tofauti na kipindi kile sisi tunacheza pia wanachama  waepukane na dhana potofu ya kuutegemea mkoa kwa ajiri ya kuendisha Timu.

“Nakumbuka mwaka 2010 Maji Maji ilipata mdhaamini lakini aliingia mitini kwa sababu ya matumizi hasi ya pesa zake ndani ya timu,hebu tujaribu kuwa wabunifu na kutafuta mbinu za kuinasua timu na sio kufuja kidogo kinachopatikana.

“Mimi nikiwa kama mjumbe wa Maji Maji baada ya uchaguzi wa hivi Karibuni ningependa kuona Timu yetu inasonga mbele na uongozi mpya ulioko madarakani usirudie makosa yaliyofanyika huko nyuma.


Makocha wa kigeni

“Wanafaa kuleta changamoto kwa makocha wazawa lakini ifikie wakati pia makocha wazawa wawezeshwe kama wa nje pindi wanapopewa nafasi, kama Nigeri walivyoweza kufanya kazi vizuri na Kocha wao Stivin Keshi nasi tuige mfano huo.


Ushauri Binafsi

“Soka la Tanzania linakufa kwa sababu ya kuitanzama Simba na Yanga lazima Tubadilike,Tff na wadhamini wazichukulie timu hizo ni timu za kawaida.

“watu wenye machungu na mpira wajaribu kuzipa udhamini na timu zingine Sio Yanga na Simba Peke yake hatuwezi kusonga mbele.


Baada ya kustaafu

“Kuanzia mwaka 1989 -1994 nikuwa nafanya kazi katika shirika la usagishaji la taifa[national milling],kuanzia hapo nilikuwa nafanya shughuli zangu za kawaida ambapo mwaka 2006 nikapata nafasi ya kuajiliwa na kampuni ya kuuza vifaa vya vipodozi pamoja na vyakula [Wadswortny Distributor],na pia ni Mjumbe wa Timu ya Maji Maji pamoja na kocha wa kambalage Veterani.


“Pia nina mke na watoto 6, Mpira umenisaidia Sana kujuana na watu ambayo ni Slaa kubwa katika maisha hata kupata kazi National Milling ni kupitia mpira ingwa soka linalipa sasa ivi kuliko enzi zetu,anaitimisha  John Kabisama mwenye umri wa miaka 58, ambaye ni shabiki wa kutupwa kabisa wa Barcelona na Maji Maji ya  Songea,ambapo katika maisha yake hawezi kumsahau Beki  wa Yanga  Elisha John kutokana na alimsumbufu wake uwanjani.

mwisho



Chapisha Maoni