MARADONA ARUDISHWA NYUMBANI KWA MATUMIZI YA MADAWA,
RONALDO KUPEWA ULINZI MKUBWA KOMBE LA DUNIA.
Na Alex Mapunda.
BRAZIL-2014
TAKRIBANI siku chache zimesalia kabla kipenga akijapulizwa kuashiria kufunguliwa kwa panzia la kombe la dunia huko nchini brazil, michuano ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na wananzi wa kandanda duniani kote , ama hakikika utakuwa ni mchike msheke wa haina yake kutokana na kwamba mataifa yote 32 hayakupata nafsi ya kushiriki michuano hiyo kwa kubahatisha.
Kombe la Dunia mara nyingi linaambatana na matukio au vituko vingi vya kushangaza kutokana na umaarufu wa michuano hiyo na watu wengi hufuatilia hatua kwa hatua,yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo yamejili kuelekea kombe la dunia pamoja na yale yaliyotokea miaka ya nyuma wakati wa kombe la dunia:-
mabaunsa wanne kumlinda Ronaldo
Shirikisho la Soka la Ureno limeomba walinzi sita kwa ajili ya safari zao mbalimbali za kujiburudisha miili yao katika fukwe za Copricabana na kwingineko. Kati ya walinzi wao, wanne watakuwa na kazi ya kumlinda Mwanasoka Bora wa Dunia kwa sasa, Cristiano Ronaldo peke yake wakati wengine watakuwa na kazi ya kulinda wachezaji wengine na viongozi wa timu hiyo. Ronaldo, Lionel Messi na Neymar wanatarajiwa kuwa mastaa wenye mvuto zaidi katika michuano hiyo kutokana na ubora wao katika ligi mbalimbali za Ulaya.
Ufaransa wataka sabuni za maji
Katika hali ya kushangaza, Ufaransa ambao wataongozwa na wakali kama Franck Ribery, Olivier Giroud, Karim Benzema na wengineo wametoa madai ya kushtusha zaidi baada ya kudai kwamba watataka sabuni za maji katika vyumba vya wachezaji wao na si sabuni za vipande.
Uongozi wa mabingwa hao wa Kombe la Dunia mwaka 1998 wanataka vyumba vyao vyote vya hoteli watakayofikia jijini Sao Paulo kuwekwa sabuni za maji na sio sabuni za vipande. Ufaransa pia wanataka hoteli yao iwe na nyama ambazo zimechinjwa kihalali kwa sababu wachezaji wao wengi ni Waislamu.
Ecuador wataka ndizi toka kwao
Timu ya taifa ya Ecuador imeandika maombi yao ya kutaka kila mchezaji wao apewe kikapu cha ndizi mbivu kutoka nchini kwao Ecuador kila siku ya michuano hiyo. Kikosi chao kinachoongozwa na mkali wa Manchester United, Antonio Valencia kinataka ndizi hizo zisafirishwe kutoka katika ardhi ya kwao Ecuador kila siku. Ndizi mbivu ni chakula maarufu kwa wanasoka wote duniani kwa ajili ya kurudisha sukari iliyopotea mwilini kutokana na mazoezi mazito ya kila siku.
Algeria wataka Kurani kila chumba
Shirikisho la Soka la Algeria limetaka kila chumba cha wachezaji pamoja na maofisa watakaoambatana na timu hiyo kuwekwa vitabu vitakatifu vya dini ya Kiislamu, Kurani kwa ajili ya maombi yao ya kila siku wakati watakapokuwa katika michuano hiyo. Kikosi chote cha Algeria kitakuwa na wachezaji Waislamu.
Hii inaashiria kuwa michuano hiyo itakuwa na mvuto wa haina yake pale itakapoanza kutimua vumbi Tarehe 13 mwaka huu katika viwanja 12 zvilivyopo katika miji mbali mbali nchini brazil huku timu nyingi tayari zimeshawaita nyota wake wanaosakata kabumbu katika timu mbali mbali duniani kote,lakini hebu tujikumbushe baadhi ya matukio ambayo yalitokea miaka ya nyuma:-
VITA YA SANTIAGO
Sahau kuhusu tukio la wachezaji wa
Argentina kupigana na wale wa
Ujerumani mara baada ya Argentina kulala kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wa robo fainali mwaka 2006. ‘ Vita ya Santiango’ ni mechi iliyokuwa ikihusisha waliokuwa wenyeji wa michuano ya mwaka 1964, Chile dhidi ya Italia. Rafu na mchezo uliotawaliwa na ubabe mwingi kutoka kwa wachezaji wa pande zote. Mwamuzi kutoka, England, Ken Aston alimpa kadi ya manjano mlinzi waItalia, Giorgio Ferrini katika sekunde ya 12 tu baada ya kuanza kwa mchezo huo.
Kufika dakika ya nane mchezaji
huyo aliondoshwa uwanjani
kwa kadi nyekundu.Ferrini, aligoma kutoka uwanjani, Polisi wakaingilia kati na baada ya dakika kumi, Ferrini alikubali kutoka uwanjani. Baadae mchezaji wa Chile, Leonel Sanchez alimpiga ngumi, Humberto Maschio wa Italia, cha kushangaza mchezaji huyo aliendelea kuwepo uwanjani na mwamuzi, Aston hakuchua uamuzi wowote. Teke la shingo kutoka kwa mchezaji, Mario David kwa Sanchez lilipelekea kadi ya pili nyekundu na hadi mwisho wa ‘ vita ya santiago’, wenyeji Chile walishinda kwa mabao 2-0.
PELE NJE YA KOMBE LA DUNIA
Mfalme wa kandanda ulimwenguni,
Pele alienda katika fainali za mwaka
1966 akiwa hayuko fiti, na wapinzani wake hasa mabeki walipata faida kubwa. Mchezo wa kwanza kati ya Brazil na Bulgaria, Pele alichezewa rafu nyingi pamoja na kufanikiwa kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 ambao, Selecao waliupata, nyota hakucheza tena hadi katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Ureno. Pele na Brazil yake wakaondoshwa katika hatua ya makundi na kurejea kwao.
ITALIA NA RUSHWA!.
Katika soka la ndani tayari klabu
kubwa za Italia zimethibitika kutoa
rushwa ili wapate matokeo. Juventus, AC Milan, Fiorentina, bila shaka mwanakandanda atakuwa anazifahamu timu hizo za ligi ya Serie A. Sakata la ‘ calciopoli’, lilipelekea Juve na Fiorentina kushushwa daraja, 2006. Lakini ni miaka mingi rushwa imekuwa sehemu ya mpira wa Italia. Katika fainali za mwaka 1974, Italia walikuwa wakihitaji pointi moja kutoka kwa Poland ambao walikuwa tayari wamefuzu kwa hatua inayofuata. Azzurri walijaribu kuwahonga Poland wauze mchezo huo, ila Poland walikataa kufanya hivyo na walipoingia uwanjani, Italia ilichapwa mabao 2-1 na kuwafanya kuondolewa kwa aibu baada ya kutaka kushinda mechi kwa mbinu chafu…
MARADONA ARUDISHWA NYUMBANI,
Nyota huyo wa zamani wa Argentina
alikuwa ameondoka Italia miaka
mitatu nyuma baada ya kugundulika kutumia madawa ya kuongeza nguvu ambazo zimekatazwa na kupigwa vita michezoni.
Maradona alitua katika fainali za
Marekani, 1994 na kuichezea nchi
yake dhidi ya Ugiriki. Alifunga bao na kutengeneza lingine katika mchezo uliofuata dhidi ya Nigeria. Siku moja kabla ya kumalizia mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Bulgaria, nyota ambaye ambaye alishangilia kwa staili iliyowatia wasiwasi wengi alipimwa vipimo vya mkojo na vilionyesha kuwa Maradona alikuwa akitumia madawa ya kulevya ya kuongeza nguvu mwilini aina ya ‘ Ephedrine’ na mara moja, FIFA ikamfukuza mashindanoni. Ulikuwa mwisho wa Argentina na Marodona kwani walipoteza mchezo wa mwisho..
RONALDO NA MATATIZO YA TUMBO,
Katika fainali ya michuano
iliyopigwa nchini Ufaransa, 1998. Brazil
ilifika fainali na kuchapwa na wenyeji mabao 3-0. Ronaldo de Lima alionekana kuwa mchovu kwa muda wote aliokuwa uwanjani. Alikuwa amepoteza nguvu nyingi, na wakati kocha wa timu hiyo Mario Zagallo alipotaja orodha ya wachezaji na kuwasilishwa kwa mwamuzi, jina la Ronaldo halikuwepo. Lilikuja kuonekana mara baada ya timu kuingia uwanjani.
Tetesi zilidai kuwa wachezaji wa
Brazil waligoma kuingia uwanjani
bila Ronaldo, huku wengine wakidai kuwa Ronaldo alicheza kwa shinikizo kutoka kwa wadhamini wake kampuni ya Nike waliolazimisha acheze. Pia ilitajwa kuwa nyota huyo alilishwa sumu kabla ya mchezo. Taarifa rasmi zilidai kuwa Ronaldo alikuwa mgonjwa na usiku wa kuamkia fainali alikuwa hospitali ambapo alipata dalili za ugonjwa wa ‘ degedege’
Yapo matukio mengine mengi
yaliyowai tokea wakati wa kombe la dunia ikiwemo Maradona kuwasurubu uingereza
kwa bao la mkono katika kombe la dunia ,yote kwa yote tusubiri mwaka huu
nchini Brazili kwa megi yatakayojili,hakika mtoto mdogo hatumwi
sokoni,Brazukaaaaa!!!!!
|
Chapisha Maoni