Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



SHAIBU KAMBANGA KIPA MAHILI WA ZAMANI WA MAJI MAJI YA SONGEA WA PILI TOKA KULIA.

 NIMFULULIZO WA MAKALA YA SHAIBU KAMBANGA MLINDA MLANGO ALIEWIKA MIAKA YA 1990 HADI 2000 AKIWA NA MAJI MAJI YA SONGEA.

ILIPOISHIA………………


 
''Mimi muda wote ambao nilicheza katika kiwango cha juu kiwango changu kilikuwa kile kile kwa kuwa nilikuwa nafuata sheria za kurinda afya nikiwa kama mchezaji,kuna kipindi  nilikaa Miezi mitatu bila kukutana na mke wangu lakini kwa wachezaji wa siku hizi ni ngumu.  

Songa nayo……………….

  Upenzi kwa Simba ni chanzo cha Maji Maji kujichinja yenyewe kwa ushirikina.



''Mwaka 1996 mzee wa timu ya Maji Maji sitamtaja jina kwa kuwa namweshimu sana alituita chumbani na kutufunika shuka nyeupe akaanza kupiga Manyanga, mimi nilikuwa nimekaa na marehemu Kisochi lemba mzee alikuwa anaongea lugha ambayo hakuna aliyekuwa anailewa lakini ilikuwa kila akipita nilipo mimi nilisika neno la mwisho akisema Maji Maji tufungwe tatu na Simba nilijaribu kumweleza mwezangu yeye akasema sio kweli ila mzee kasema Maji Maji tushinde tatu,niliendelea kumsikiliza yule mzee kwa makini sana na baada ya tukio lile nilijalibu kuwaeleza wenzangu wote walishangaa.



 ''Tukaja kwenye mechi mchezo ulikuwa mgumu sana upande wetu na kama yule mzee nilivyomsikia mimi Simba walifunga bao 3-0 na yule Mzee ni mwanachama hai wa Simba Mwenye kadi.





''Na mara nyingi ilikuwa Siku ya Mechi na Simba Wachezaji wa Maji Maji walikuwa wakituwekea dawa kwenye chakula ili kutupunguza nguvu.


“Mechi zote ambazo tulikuwa tunacheza na Simba chakula alikuwa anapika Yule Mzee ambaye ni Mganga wetu lakini mechi zingine alikuwa anapika mtu mwingine,nakumbuka siku ambayo alituombea kufungwa dhidi ya Simba alituwekea dawa kwenye chakula ili kutupunguza nguvu,kutokana na tukio lile Masaa machache kabla ya Mchezo mwezetu John Alex aliamua kuchukua vifaa vyake na kurudi nyumbani,hali ambayo hakuna mtu yeyote ambaye alishituka na baada ya mchezo tukakung’utwa na Simba huku wachezaji tukiwa hoi.

Atoboa siri ya Maji Maji kuwa kibonde kwa Simba.



  ''Asilimia 90 ya viongozi wa Maji Maji ni mashabiki na wadau wa Simba hadi hivi sasa hali ambayo inapelekea Maji Maji kufungwa Nyumbani na ugenini huku wakijikakamua  sana ni sare mara nyingi simba inapofika Songea toka miaka ya 1990,maandalizi yanakuwa afifu sana na tatizo kubwa ni ushabiki wa viongozi
.
Itaendelea kesho tarehe 06-05-2014 ambapo atasimulia sababu ya yanga kufungwa mara kwa mara katika uwanja wa Maji Maji na Wanalizombe.
Usikose………………


Chapisha Maoni