Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






Na Alex Mapunda,Iringa
BAADA ya kindumbwe ndumbwe cha ligi daraja la kwanza kumalizika salama na timu zilizopanda ligi kuu kufahamika  macho na masikio ya wadau wa soka hapa nchini yanataka kuona na kusikia jinsi timu hizo zitakavyo leta upizani katika ligi kuu ya Vodacom kutokana na historia ya timu zote nne katika ligi kuu miaka ya nyuma.
Timu hizi tunaweza kusema kuwa licha ya uwezo ambao zilionyesha ndani ya uwanja pia zimebebwa na historia  ambayo zilijiwekea miaka ya nyuma katika ligi ambapo baadhi ya timu hizo zilicheza kwa mafanikio makubwa.
majimaji Sc ‘wanalizombe’
 
maji maji ambayo ilianzishwa mwaka 1977 ilipata umaarufu mkubwa mwaka 1980, mwaka ambao timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza ligi daraja la kwanza ambayo kwa sasa ni ligi kuu.
Kutokana na kusheheni wachezaji wenye vipaji kama piter mhina,John Kabisama,Isihaka Majaliwa,Madaraka Suleiman, ilipelekea timu hiyo kuwa tishio na kuchua kombe la muungano mwa 1985,1986 na 1998 na kuwakilishwa nchi katika michuano ya klabu bingwa Africa.
Kwa mara ya mwisho Maji Maji ilishuka daraja  mwaka 2010 na sasa imerejea tena katika ligi kuu ambapo  mashabiki wengi wa soka nchini wanaikumbuka maji maji ya songea maarufu kwa jina la wanalizombe na wanaamini timu hiyo itakuwa tishio kama itajipanga vizuri.
African sport ‘wanakimanumanu’




Ni miaka takribani 23 sasa tangu klabu bingwa ya zamani ya Tanzania, african sports club iliposhuka daraja  na sasa imerudi tena ligi kuu kwa kishindo baada ya kuongoza kundia A kwa kufikisha pointi 48 ambapo Timu hiyo iliwai kufanya vizuri miaka ya 1980 hadi 1990  na kujiwekea heshima kubwa dhidi ya   mpinzani wake coastal union  na Tanzania kwa ujmla.

African sports ilitwaa kombe la ligi  mwaka 1988  lakini ikashuka  daraja mwaka 1991 .urejeo wa timu hiyo unawakumbusha wengi pambano la mwisho mwaka 1988 ambalo lilimalizika kwa sports kuishinda coastal kwa magoli 2-0.
Timu hiyo inaitaji kupambana ili kuleta ushindani katika ligi kama ilivyokuwa  zamani na tayari Tanga kuna timu tatu Coastal Union,Mgambo pamoja na African Sports hakika ushindani utakuwa mkubwa.
Toto africans ‘wanakishamapanda’
 
Toto africans imepanda ligi kuu baada ya juhudi za muda mrefu. klabu hiyo ilishuka daraja kutokana na ukata ulioikabili mwaka 2013. kabla ya kushuka daraja miaka miwili iliyopita, toto ilikuwa imecheza misimu sita mfululizo kwani ilikuwapo kwenye ligi tangu msimu wa 2007/08. hivi sasa timu inaongeza utamu wa soka kwa kanda ya ziwa baada ya kagera sugar, stand united na mwadui nao kuwa na nafasi kwenye ligi.
kocha mkuu wa toto, John Tegete  baada ya kupanda alisema, “ kilichotubeba kupanda ligi kuu ni usajili mzuri, licha ya umaskini wa timu yetu tulitafuta wachezaji bora wenye viwango na uzoefu mzuri.”alisema Tegete.
Toto African ni Timu zuri lakini mara nyingi inashindwa kufanya vizuri kutokana na kujiingiza katika mlengwa wa Simba na Yanga hali ambao inapelekea kuibuka matabaka ndani ya timu hiyo.
mwadui fc[wazee wa madini]


Mwadui Fc kifedha wako vizuri na wako chini ya udhamini wa mgodi wa almasi wa petra diamonds -wiliamson uliopo mwadui shinyanga. timu hii ilitamba msimu uliopita kwenye ligi daraka la kwanza, lakini ikashindwa kwa pointi mbele ya majirani zao stand united.
mwadui fc ni moja ya timu kongwe nchini, ilicheza ligi kuu kati ya miaka ya 70 na kisha kushuka kwenye miaka ya 80.
moja ya mafanikio ya timu hiyo ni kufika nusu fainali ya kusaka ubingwa wa Tanzania kwa kuitoa yanga kwa mikwaju ya penalti.
kocha mkuu wa mwadui fc, jamhuri kiwhelo ‘julio’ ni moja ya watu muhimu walioiletea mafanikio makubwa timu hiyo kutokana na uwezo wake wa kufundisha pia kusajili wachezaji wenye vipaji na wakongwe kama Athumani Iddi,Uhuru Sulemani pamoja na Razack Khalfani  na  amehaidi kusajili wachezaji wazuri zaidi ili kuijenga timu hiyo na kurudisha makali yake ya miaka ya nyuma.
Ni ukweli usiopingika kuwa timu hizo zilipigana sana na zilifanya usajili mzuri ambao uliwaghalimu pesa kubwa na kikubwa timu hizo zisibweteke na sifa ambazo zimepata toka kwa wadau za kupanda ligi kuu badala yake ni kujipanga ili kukabiliana na fitina za Simba na Yanga kikamilifu.


Chapisha Maoni