Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Nyota wa Colombia James Rodriguez

Nyota wa Colombia na Monaco James Rodriguez alidhibitisha kuwa anajua  katika kombe la dunia alipofunga mabao mawili na kuisaidia Colombia kuwa timu ya pili kufuzu kwa nane bora .
Rodriguez mwenye umri wa miaka 22 alikuwa nyota katika safu ya ushambulizi ya Colombia ilipokuwa ikichuana dhidi ya Uruguay bila mshambulizi wake mwenye utata Luiz Suarez.
Bila shaka mshambulizi huyo sasa atakumbukwa katika mizani sawa na Neymar wa Brazil na Lionel Messi wa Argetina nyota wa Brazil2014 watakapokuwa wakitajwa haswa kutokana na miondoko yake hapo jana katika uwanja wa Rio.Wengi wanaashiria kukosekana na Suarez kuwa kisababu cha kikosi cha Oscar Tabarez kushindwa kusonga mbele katika kipute hicho kinachoendelea huko Brazil.
Mchezaji huyo wa Monaco alitangaza kuwepo kwake uwanjani kwa mkwaju wa dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza uliomwacha kipa ya Uruguay Fernando Muslera ameduwaa huku maelfu wa mashabiki wa Colombia wakishangilia kwa nusia tikiti ya Robo fainali ya kombe la dunia .


Nyota wa Colombia James Rodriguez anatarajiwa kuibabashia Brazil
Rodriguez hakuachia hapo, aliendelea kuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Vijana wa Oscar tabarez na juhudi zake zikazaa matunda kunako dakika ya 58 Mshambulizi huyo alipofuma bao la pili na ushindi na kuahakiki nafasi hiyo ya nane bora kwa Colombia.
Kufuatia matookeo hayo sasa Colombia watachuana na wenyeji Brazil katika mechi inayotazamiwa na wengi kuwa ngumu ya kuwania nafasi ya nusu fainali.
Mechi hiyo itachezwa siku ya ijumaa katika uwanja wa Fortaleza .
Uruguay ilikosa keke zake za kawaida katika mechi hii ilikuwa bayana kuwa japo Suarez hakuwepo uwanjani mashabiki wake walimsifia na kubeba mabango y kumuunga mkono mshambulizi huyo wa Liverpool ya Uingereza .
Washambulizi wake Maximiliano Pereira na Edinson Cavani fndio waliomjaribu kipa wa Colombia David Ospina.


Chapisha Maoni