Mchezaji wa kitambo wa Brazil
ana wasiwasi kuwa taifa hilo linamshinikiza mshambulizi wa Neymar
kuisaidia taifa hilo kunyakua taji la Kombe la Dunia kwa wenyeji hao na
huenda ikamkosesha mshambulizi huyo machachari wa Barcelona umakini.
Neymar mwenye umri wa miaka 22 hajawahi
kushiriki Kombe la Dunia lakini amefunga jumla ya mabao 7 kati ya
michuano 9 iliyocheza na kushinda Brazil hivyo Ni mzigo mkubwa sana kwake kuachiwa majukumu yote.”Brazil wamewahi kushinda Kombe la Dunia mara tano lakini hawajashinda taji hilo tangu mwaka wa 2002.
Wenyeji hao ambao watachuana na Croatia katika mechi ya kwanza ya mashindano hayo jijini Sao Paulo siku ya Alhamisi, walishinda kombe la Mashirika la mwaka wa 2013 kwa kuwalaza mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Uhispania mabao 3-0 katika fainali.
Timu hiyo inayoongozwa na Luiz Felipe Scolari pia imeshinda mechi tisa za kirafiki kwa mpigo tangu waliposhindwa na Uswizi mwezi Agosti, huku wakifunga jumla ya mabao 30 na kufungwa 2 tu.
“Kwa mara ya kwanza katika historia, Brazil ina safu nzuri ya ulinzi kuliko safu ya ushambulizi,” alisema Pele mwenye umri wa miaka 73, mfungaji bora zaidi wa mabao wa timu yake ya taifa kwa mabao 77.
“Kiungo cha kati kiko sawa.
Wamejipanga sawasawa.
Natumai tutarekebisha kuanzia safu ya kati hadi ya ushambulizi.”
BY BBC NETWORK
Chapisha Maoni