Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




TIMU ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kufunzu katika hatua ya pili ya mtoano baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya bao 3-2 baada ya kutoka sare ya bao 2-2 katika mechi ya marudiano nchini Zimbabwe.



Bao la dakika ya 10 walilopata Zimbabwe kupitia kwa Phiri Danisa liliwashitua mashabiki wa Tanzania, lakini nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub Canavaro katika dakika ya 21 aliwazishaa bao hilo na kuufanya ubao wa matangazo kusomeka 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.


Wakati Zimbabwe wakiwa katika presha ya kusaka bao la pili, dakika ya 46 kipindi cha pili walifanya makosa na Thomas Emmanuel Ulimwengu hakufanya makosa na kuwaadhibu goli la pili kabla ya 55 kipindi hicho cha pili, Katsande Willard aliifungia Zimbabwe bao la pili la kusawazisha.


Kwa matokeo ya leo, Taifa stars imefuzu hatua ya mwisho ya mtoano kwa wastani wa mabao 3-2 
kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika.


Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza na matokeo ya 2-2 mjini Harare ambapo sasa taifa stars itakutana na Msumbiji katika hatua ya mwisho ya mtoano.



STARSULIMWENGUU


Chapisha Maoni