Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mchezaji  wa Argentina,Angel Di Maria kuna uwezekano wa kukosa mechi ya nusu fainali Jumatano ijayo kati ya Argentina na Uholanzi.
Hi ni baada ya mchezaji huyo kupata jeraha la Paja wakati wa mechi yao dhidi ya Ubelgiji ambapo walishinda bao moja bila.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alilazimika kupumzika baada ya dakika 33 ya kipindi cha kwanza cha mechi nchini Brazil baada ya kujeruhiwa alipokuwa anapiga shuti.
Kocha Alejandro Sabella alinukuliwa akisema: "Angel ana tatizo la Paja lake la kulia na kwamba atachunguzwa zaidi.
Di Maria aliingiza bao la ushindi katika mechi yao dhidi ya Switzerland katika awamu ya muondoano.
Enzo Perez wa Benfica alichukua nafasi yake katika mechi dhidi ya Ubelgiji.

  1. Born: February 14, 1988 (age 26), Rosario, Argentina
  2. Weight: 75 kg
  3. Salary: 3 million EUR (2012)
  4. Current teams: Argentina national football team (#7 / Midfielder), Real Madrid C.F. (#22 / Midfielder)
  5. Nationality: Argentine, Italian


Chapisha Maoni