Mziki wa kizazi kipya hapa nchini adi
leo hii toka walipoibuka akina Joseph Haule umevuka mabonde na milima huku
wakiibuka wasani wapya wengi lakini pia wakonge wengi wakizidi kupotea katika
mziki .
Lakini Kwa sasa msanii Diamond ndiye
msanii ambaye ameteka soko la mziki hapa nchini kutokana na kufanya nje shoo
nyingi na wasanii wakubwa kama Davido,pia amedhihirisha umwamba baada ya hivi
karibuni kutwaa tuzo nyingi ambazo zinaandaliwa na kill music award na
kuwafunika wezake..
Katika
tuzo hizo Diamond aliweza kuvunja rekodi
kwa kuibuka kidedea kwa zaidi ya tuzo 6 kwa vipengele tofauti alivyoshiriki
ikiwemo mtunzi bora wimbo wa kizazi kipya,mtumbuizaji bora wa kiume,video bora
ya mwaka kwa wimbo wa my number one,muziki bora wa mwaka,muimbaji bora wa kiume
wa kizazi kipya na wimbo bora wa Afro
pop.
Waliofuatia
kwa tuzo zaidi ya moja ni Mzee Yusuf kwa tuzo
nne ikiwemo moja kundi bora la muziki wa Taarabu,Mashujaa band tuzo
mbili kwa kuwa bendi bora ya mwaka na wimbo bora wa bendi wa mwaka wa
Kiswahili,Fid Q amepata tuzo ya mtunzi bora wa Hiphop na msanii bora wa
Hiphop,Lady Jaydee amepata tuzo ya wimbo bora wa Zhouk na mwimbaji bora wa kike
wa kizazi kipya.
Walioambulia
tuzo mojamoja ni Chibwa akiwa mtunzi bora wa Rege,wimbo bora wa rege ni DOUBLE
BOO,muziki wenye vionjo vya asili ni Da Bongo massive,Young Killer ni msanii
bora chipukizi,Christian Bella ni mtunzi bora wa kizazi kipya katika
bendi,Enrico ni mtayarishaji bora wa nyimbo za taarabu,Amorosso ni mtayarishaji
bora wa nyimbo katika bendi,Niki wa 2 nyimbo bora ya mwaka ya hiphop[nje ya
box],Ney wa mitego na Diamond ni wimbo bora wa kushirikiana [muziki gani],Jose
Chamelion ni wimbo bora wa Afrika Mashariki [tubonge],Man Walter ni
mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya,Hassan Bitchuka amepata tuzo ya
heshima,Isha Ramadhanii ni mtumbuizaji bora wa kike,Ferguson ni rapa bora
katika bendi,kikundi bora cha mwaka kizazi kipya ni Weusi,wimbo bora wa RnB ni
wa Vanessa Mdee[crazy] na muimbaji bora wa kike katika bendi ni Luiza Mbutu.
Tuzo
za Kilimanjaro Music Award hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukuza na kuongeza
ufanisi na hamasa kwa wasanii,watunzi na watayarishaji wa muziki ili
kuhakikisha unasonga mbele hapa ambapo mwaka huu kulikuwa na vipengele
vipatavyo 36 vilivyoshindaniwa vilivyowafanya wasanii walichopanda na kukivuna
huku Diamond akiwa gumzo kwa kubeba tuzo sita.
Hakika
kwa wasanii wengine wanatakiwa kufuata nyayo zake ili kufikisha mziki wa hapa
nchini kimataifa ambapo diamond amekuwa maarufu zaidi baada ya nyota yake kung'aa kimataifa na anazidi kuchanja mbuga.
Chapisha Maoni