LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumapili Machi 8
Mgambo JKT v Ndanda FC
Mtibwa Suga v Mbeya City
Simba v Yanga
Jumanne Machi 10
Polisi Moro v Ruvu Shooting
Katika idadi hiyo Simba inaongoza kwa kushinda mara nne na Yanga ikipata ushindi mara tatu na mara nne zikienda sare lakini kizuri kwa Yanga ni kuwa na bahati kushinda Oktoba
OKTOBA 18 uwanja wa taifa Dar es
Salaam kutawaka moto wakati miamba ya soka Tanzania klabu za Yanga na Simba
zitakapomenyana kuwania pointi tatu muhimu ikiwa ni mara ya kwanza timu hizo
kukutana tangu kuanza kwa msimu huu.
Timu hizo mbili zimekuwa na upinzani
mkubwa tangu zilipoanzishwa miaka ya 1935 na 1936,kitu ambacho kimechangia
kuwepo uhasama mkubwa na kusababisha kugawana bara bara.
MECHI 5 ZILIZOPITA ZA MISIMU MITATU:
Yanga
1-1 Simba
Simba
0-2 Yanga
Simba 3-3 Yanga
Yanga
1-1 Simba
Yanga
0-0 Simba
Takwimu kuanzia timu hizo zilipoanza
kukutana zinaonyesha Yanga ndiyo kinara kwa kupata ushindi mara nyingi zaidi ya
Simba ambayo inafuatia kwa mbali.
Takwimu kama hizo kwenye upande wa
kunyakua ubingwa wa Tanzania bara pia zinaibeba Yanga kwa kuchukua ubingwa huo
mara 24 wakati Simba ikifanya hivyo mara 18 na kufuatiwa na klabu za Mtibwa
Sugar na Coastal Union ya Tanga.
Rekodi nzuri kwa Simba katika
mapambano yake na Yanga ni kupata ushindi wa mabao mengi kama ilivyofanya mwaka
1977 iliweza kuifunga Yanga mabao 6-0 na Mei 6 mwaka 2012 iliipa tena kipigo
cha aibu cha mabao 5-0,uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Simba imekuwa makini kwa kutumia
vizuri madhaifu yawapinzani wao inapo wakuta wamechoka na kufunga mabao mengi
yanayowapa rekodi nzuri kwenye historia za timu hizo.
Takwimu za Jelamba viwanjani za miaka
mitano iliyopita kuanzia 2009 zinaonyesha Simba na Yanga zimekutana mara 11
ikiwa ni mechi maalumu pamoja na zile za Ligi Kuu ya Tanzania bara.
Katika idadi hiyo Simba inaongoza
kwa kushinda mara nne na Yanga ikipata ushindi mara tatu na mara nne
zikienda sare lakini kizuri kwa Yanga ni kuwa na bahati ya kupata ushindi
inapokutana na Simba mwezi Oktoba.
Oktoba 16 mwaka 2010 pambano la Ligi
Kuu Tanzania bara lilifanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Yanga
iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Jeryson Tegete dakika ya 70.
Yanga ilifanya tena hivyo Oktoba
29/2011 kwa kuifunga Simba safari hii ikiwa uwanja wa taifa Dar es Salaam
mfungaji akiwa Mzambia Davis Mwape dakika ya 75,na msimu uliofuata kidogo
vijana wa Msimbazi waligoma kufanywa wateja baada ya kukutana Oktoba 3/2012 na
kutoka sare ya 1-1 na Yanga Simba wakitangulia kufunga kupitia kwa Amri
Kiemba dakika ya tatu na Yanga ikasawazisha dakika ya 64 kupitia kwa Said
Bahanuzi.
Oktoba 20,2013,Simba iligoma
kwa mara nyingine kufungwa na Yanga kwenye mwezi huo baada ya kulazimisha sare
ya mabao 3-3 huku yenyewe ikitoka nyuma ka mabao matatu yaliyofungwa kipindi
cha kwanza na Yanga.
Wafungaji wa Yanga katika mechi hiyo
walikuwa ni Mrisho Ngasa aliyefunga bao la kwanza dakika ya 14 na Mganda Hamisi
Kiiza aliyefunga mara mbili dakika ya 35,47
Mabao ya Simba yalifungwa na Beatram
Mwombeki dakika ya 53Joseph Owino dakika ya 5 na Mrundi Gilbert Kaze dakika ya
83 mechi hii ikiwa maalumu ikipewa jina la Nani Mtani Jembe.
Ushindi pekee iliyowahi kuupata
Simba inapocheza na Yanga ndani ya miaka mitano iliyopita ilikuwa ni Oktoba 31
ambapo iliweza kuifunga Yanga bao 1-0 mfungaji akiwa Mussa Hassani Mgosi dakika
ya 26.
Katika takwimu hizi zilizowekwa na
Mtandao wa Goal kila timu inacho cha kujivunia katika pambano hilo la Jumamosi
Simba imekuwa na kipindi kizuri katika miaka mitano iliyopita wakati Yanga
ikifurahi kukutana na Simba mwezi Oktoba kwa sababu imekuwa na bahati nao.
Lakini wakato Goal inakuwekea rekodi
hizo timu husika kwa sasa zipo katika maandalizi kabambe kujiandaa na pambano
hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka.
Yanga ambao ndiyo wenyeji wa pambano
hilo licha ya kufurahia kucheza mwezi Oktoba lakini wanajivunia matokeo yao ya
ushindi katika mechi mbili zilizopita dhidi ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons
ambayo yamewaweka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Simba iliyokuwa imeweka kambi nchini
Afrika Kusini bado mambo siyo shwari kwani haijaonja ladha ya ushindi katika
mechi tatu ilizo cheza ligi ya msimu huu.
Kocha wake Patrick Phiri,amesea
anauchukulia mchezo huo kama fainali lengo lake likiwa ni kupata ushindi ili
kurudisha matumaini ya kunyakua ubingwa.
Ikumbukwe timu hiyo haijafanya
vizuri katika misimu miwili iliyopita ambapo msimu wa 2012/13 ilimaliza nafasi
ya tatu na msimu wa 2013/14 ikamaliza nafasi ya nne na msimu huu imetumia fedha
nyingi kwa ajili ya kusajili wachezaji wenye majina na viwango vya juu ili
kuweza kushinda taji hilo lakini inaonekana bado mambo hayaja kaa sawa.
Pia timu hiyo mbali na kupata sare
hizo tatu lakini haijaonyesha kiwango cha juu kiasi cha kuwaridhisha mashabiki
wake ambao wanafika wachache uwanjani lakini katika mechi ya Jumamosi chochote
kinaweza kutokea.
Tusubiri kipyenga cha Mwamuzi Israel
Nkongo ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha pambano hilo takika zake 90
zitamalizika kwa timu gani ikiwa na furaha.
Takwimu
muhimu za Yanga na Simba
OKTOBA 18 uwanja wa taifa Dar es
Salaam kutawaka moto wakati miamba ya soka Tanzania klabu za Yanga na Simba
zitakapomenyana kuwania pointi tatu muhimu ikiwa ni mara ya kwanza timu hizo
kukutana tangu kuanza kwa msimu huu.
Timu hizo mbili zimekuwa na upinzani
mkubwa tangu zilipoanzishwa miaka ya 1935 na 1936,kitu ambacho kimechangia
kuwepo uhasama mkubwa na kusababisha kugawana bara bara.
Takwimu kuanzia timu hizo zilipoanza
kukutana zinaonyesha Yanga ndiyo kinara kwa kupata ushindi mara nyingi zaidi ya
Simba ambayo inafuatia kwa mbali.
Takwimu kama hizo kwenye upande wa
kunyakua ubingwa wa Tanzania bara pia zinaibeba Yanga kwa kuchukua ubingwa huo
mara 24 wakati Simba ikifanya hivyo mara 18 na kufuatiwa na klabu za Mtibwa
Sugar na Coastal Union ya Tanga.
Rekodi nzuri kwa Simba katika
mapambano yake na Yanga ni kupata ushindi wa mabao mengi kama ilivyofanya mwaka
1977 iliweza kuifunga Yanga mabao 6-0 na Mei 6 mwaka 2012 iliipa tena kipigo
cha aibu cha mabao 5-0,uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Simba imekuwa makini kwa kutumia
vizuri madhaifu yawapinzani wao inapo wakuta wamechoka na kufunga mabao mengi
yanayowapa rekodi nzuri kwenye historia za timu hizo.
Takwimu za Goal za miaka mitano
iliyopita kuanzia 2009 zinaonyesha Simba na Yanga zimekutana mara 11 ikiwa ni
mechi maalumu pamoja na zile za Ligi Kuu ya Tanzania bara.
Katika idadi hiyo Simba inaongoza
kwa kushinda mara nne na Yanga ikipata ushindi mara tatu na mara nne
zikienda sare lakini kizuri kwa Yanga ni kuwa na bahati ya kupata ushindi
inapokutana na Simba mwezi Oktoba.
Oktoba 16 mwaka 2010 pambano la Ligi
Kuu Tanzania bara lilifanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Yanga
iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa Jeryson Tegete dakika ya 70.
Yanga ilifanya tena hivyo Oktoba
29/2011 kwa kuifunga Simba safari hii ikiwa uwanja wa taifa Dar es Salaam
mfungaji akiwa Mzambia Davis Mwape dakika ya 75,na msimu uliofuata kidogo
vijana wa Msimbazi waligoma kufanywa wateja baada ya kukutana Oktoba 3/2012 na kutoka
sare ya 1-1 na Yanga Simba wakitangulia kufunga kupitia kwa Amri
Kiemba dakika ya tatu na Yanga ikasawazisha dakika ya 64 kupitia kwa Said
Bahanuzi.
Oktoba 20,2013,Simba iligoma
kwa mara nyingine kufungwa na Yanga kwenye mwezi huo baada ya kulazimisha sare
ya mabao 3-3 huku yenyewe ikitoka nyuma ka mabao matatu yaliyofungwa kipindi
cha kwanza na Yanga.
Wafungaji wa Yanga katika mechi hiyo
walikuwa ni Mrisho Ngasa aliyefunga bao la kwanza dakika ya 14 na Mganda Hamisi
Kiiza aliyefunga mara mbili dakika ya 35,47
Mabao ya Simba yalifungwa na Beatram
Mwombeki dakika ya 53Joseph Owino dakika ya 5 na Mrundi Gilbert Kaze dakika ya
83 mechi hii ikiwa maalumu ikipewa jina la Nani Mtani Jembe.
Ushindi pekee iliyowahi kuupata
Simba inapocheza na Yanga ndani ya miaka mitano iliyopita ilikuwa ni Oktoba 31
ambapo iliweza kuifunga Yanga bao 1-0 mfungaji akiwa Mussa Hassani Mgosi dakika
ya 26.
Katika takwimu hizi zilizowekwa na
Mtandao wa Goal kila timu inacho cha kujivunia katika pambano hilo la Jumamosi
Simba imekuwa na kipindi kizuri katika miaka mitano iliyopita wakati Yanga
ikifurahi kukutana na Simba mwezi Oktoba kwa sababu imekuwa na bahati nao.
Lakini wakato Goal inakuwekea rekodi
hizo timu husika kwa sasa zipo katika maandalizi kabambe kujiandaa na pambano
hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka.
Yanga ambao ndiyo wenyeji wa pambano
hilo licha ya kufurahia kucheza mwezi Oktoba lakini wanajivunia matokeo yao ya
ushindi katika mechi mbili zilizopita dhidi ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons
ambayo yamewaweka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Simba iliyokuwa imeweka kambi nchini
Afrika Kusini bado mambo siyo shwari kwani haijaonja ladha ya ushindi katika
mechi tatu ilizo cheza ligi ya msimu huu.
Kocha wake Patrick Phiri,amesea
anauchukulia mchezo huo kama fainali lengo lake likiwa ni kupata ushindi ili
kurudisha matumaini ya kunyakua ubingwa.
Ikumbukwe timu hiyo haijafanya
vizuri katika misimu miwili iliyopita ambapo msimu wa 2012/13 ilimaliza nafasi
ya tatu na msimu wa 2013/14 ikamaliza nafasi ya nne na msimu huu imetumia fedha
nyingi kwa ajili ya kusajili wachezaji wenye majina na viwango vya juu ili
kuweza kushinda taji hilo lakini inaonekana bado mambo hayaja kaa sawa.
Pia timu hiyo mbali na kupata sare
hizo tatu lakini haijaonyesha kiwango cha juu kiasi cha kuwaridhisha mashabiki
wake ambao wanafika wachache uwanjani lakini katika mechi ya Jumamosi chochote
kinaweza kutokea.
Tusubiri kipyenga cha Mwamuzi Israel
Nkongo ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha pambano hilo takika zake 90
zitamalizika kwa timu gani ikiwa na furaha.
MATOKEO:
Jumamosi Machi 7
Coastal Union 2 Kagera Sugar 2
JKT Ruvu 0 Azam FC 1
Chapisha Maoni