Sehemu ya mwisho ya historia ya maisha ya soka ya Kelvin Yondani mzaliwa wa mwanza ambaye alicheza simba na reli ya morogoro kiboko ya vigogo.
ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“Basi kutokana na tuuma ile na licha
ya kwamba kiwango changu kilikuwa kikubwa masikini ya mungu sikupewa nafasi
hata ya kusafiri na timu kwenda nchini Msumbiji katika mechi ya marudiano
waliniacha Bongo.
“Kuanzi hapo nilichukiwa sana hadi
nikahasirika kisaikorojia pindi nikiwapo uwanjani lakini ukweli ni kwamba mimi
sikuwa na mapenzi na Yanga na kukosa Bao ni suala la kawaidi kwa mchezaji sio
makusudi.
songa nayo
Waamzi.
“Viwango vyao vipo chini sana
hawjiamini pindi wawapo uwanjani kutokana na kupokea Takribani toka pande
mbili hali hiyo inapelekea wachezaji kuchezeana rafu mbaya na mwamzi anajifanya
haoni.
“Mfano kuna tukio lilitokea Hivi
karibuni la Haruna Moshi Boban kumchezea Rafu mbaya Kelvin Yondani
[Yanga]mwamzi badala ya kutoa kadi nyekundu akatoa kadi ya njano huu ni uzembe
mkubwa kwa waamzi wetu lazima wabadilike.
Katiba.
“TFF lazima wafanyie mabadiliko ya
katiba ya soka hapa nchini hasa kipengere cha uchaguzi badala ya wanachama
wachache kumchagua kiongozi wa chama wa ngazi ya chini au ya juu badala yake
achaguliwe na umaa, ili kuepuka tatizo la watu wachache wenye pesa wasiojua
mpira kuchukua madarada kwa kuwaonga wapiga kura.
“Kuna kipindi nilijisikia aibu sana
wakati nilipoenguliwa mwaka 2005 katika nafasi ya ujumbe Ilemela na wakampa mtu
kutokana na vijiela vyake ambaye hajue chochote kuhusu mpira kunishinda mimi.
Wachezaji anaowakubali
“Namkubali sana Haruna Niyonzima
kiungo wa Dar Es Salam Yang Afrika yupo Vizuri kwa ukanda huu wa afrika mashariki
na kati, lakini sio kwamba napendelea ni ukweli ni Mtoto wa kaka yangu Kelvini
Yondan Anafanya vizuri katika nafasi ya Ulinzi kwa hivi sasa hapa nchini.
Kipa Msumbufu.
“Mwameja huyu ni balaa mimi nadiriki
kusema kuwa hakuna mlinda mlango ambaye hadi hii leo amefikia uwezo wa Mwameja.
“Mimi alikuwa akinisumbua sana ,mara
nyingi mazoezini alikuwa anawaita na kuwawekea mpira eneo la penalti na
kuwaambia atakayefunga penalti tano nampa fedha,lakini matokeo yake unaishia
tatu au mbili,mimi sikuwai shuhudia Mwameja akifungwa Penalti 5.
Ushauri kwa Timu ya Taifa.
“Hata ashuke Yesu, kwa mfumo
wanaoutumia Taifa Stars na haina ya wachezaji walionao kushiriki kombe la dunia
ni ndoto,lazima yafanyike mabadiliko makubwa sana ili kunusuru soka letu.
“Mimi kipindi nacheza nilikuwa na
nguvu sana hizo nguvu za Thomas Ulimwengu ambaye ni nchezaji mwenye nguvu kwa
kipindi hiki hata robo kwangu hatii ndani,wachezaji wa kipindi chetu
walikuwa na vitu vingi sana ni mchezaji gani? Wa sasa ivi ana uwezo wa
kumwamisha beki kwenye Reli na kupasia wavu,hakuna.
“wachezaji wenye vipaji vya
kweli tunawacha na badala yake tunawakumbatia wachezaji wasio na akiri ya
uwanjani,Tff wanakijua cha kufanya.
Baada ya kustaafu.
“Kwa sasa nina miaka 48,nina mke na
watoto wawili ,najisughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa pamoja udalali wa
kutafuta Bidhaa Mbali mbali Zinazopatikana hapa Mwanza kwenda Dar na mke
wangu ajishughulisha na ufugaji wa Kuku wa kisasa maisha yetu Sio mabaya.
“kwa kweli sikunufaika na mpira
kiuchumi ila kuwa maarufu na kufahamiana na watu imenisaidia sana kufanya
shughuli zangu kwa uraisi,Anahitimisha Yondani ambaye ametokea katika ukoo wa
wachezaji wa ukweli wa soka na watoto wake muda wote anawahamasisha kuhusu
mpira,na wanacheza vizuri.
Chapisha Maoni