Sophia Mwaipyana,Mbeya
Timu ya kimondo Sc ya wilayani mbozi mkoani hapa inayoshiriki ligi daraja la kwanza imewataja wachezaji 15 ambao wataendelea kuitumikia timu hiyo na
wachezaji walio watema katika kikosi
hicho .
Akizungumza na Championi Juma tatu katibu msaidizi wa timu hiyo Silla Yalonde
amesema wameamua kubakiza wachezaji 15 na watasajiri wengine ambao watajulikana
hapo baadaye baada usajiri kukamilika hii ni kutokana na pendekezo la benchi la
ufundi ambalo linahitaji kikosi kidogo cha watu wachache lakini chenye ufanisi
mkubwa kwani wanajipanga vizuri kwaajili ya kupanda ligi kuu.
Yalonde amewataja wachezaji hao kuwa ni Azishi Saimoni Petro,Emamanuel
OthmanChacha,Meshack Simbeye, Baraka Mtafya,Casmir Frank Mwamboka,Mashaka David
Mwakyoma,,Job Sichone,Issa Kapweka,Asifiwe Lwinga, Geofrey Mwashiuya,Bright
Berbatov Sichalwe,Mwamba Mkumbwa,Geofrey Mine Mlawa,Joshua Omary Ally na
Patrick Mangungulu.
Aidha amewataja wachezaji walioachwa na timu hiyo kwa sababu mbalimbali
ikiwemo kwenda masomoni, kushuka viwango na kumaliza mikataba yao kuwa ni
Ramadhani Hussein Sangai, Twaha Zubeiry Mageha,Daudi Martin Mwaipyana, Guna
Benedict Miho, Patrick Mwitilila Mwamengo, Rodgers Mwaisoloka,Joel Kasimila,Abu
Suwilanji Mwamengo,Afrika Junior Simbeye, Daudi Mafufu Mwanja, John
Mwanji,Charles Hizza, Christopher Kassewa,Sille Sanga,na Amirson Mohamed Bori.
Pia ameongeza kuwa wachezaji walibaki
katika timu wameanza kambi leo na ambao hawaja fika wametakiwa kuingia kambini
kwaajili ya kuanza mazoezi na kocha ili wajipange vizuri kwa msimu ujao.
Amewataka wadau wa soka kujitokeza
kwa wingi kuisapoti timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuiombea timu hiyo ifanye
vizuri pia kufadhiri timu hiyo kwa hali na mali pia mawazo ili timu hiyo iweze
kupanda daraja na kushirikiligi kuul.
Chapisha Maoni