Timu ya soka ya maji maji toka mkoani Ruvuma imesajili
wachezaji wapya sita wakiwemo wawili toka kwa wapinzani wao Mlale JKT ili
kuimarisha kikosi chao kabla ya michuano ya ligi Daraja la kwanza kuanza
kutimua vumbi kwa nchini zima.
Wachezaji ambao wamesajiliwa toka Jkt Mlale ni Mkongwe
aliyepata kuweka hapa nchini Kudra omari pamoja na Idd Kipagwile,wachezaji
wengine waliosajiliwa toka nje ya mkoa wa Ruvuma ni Ally Hassan,David
Abdallah,Yusuph mgwao pamoja naSaid zeco ambapo wataongezez nguvu kikosi hicho.
Akizungumza na championi Ijumaa Meneja wa timu hiyo Good
Mvula alisema kikosi hicho kitaingia kambini,jumatatu mjini songea kabla ya
kambi hiyo kuamishia katika mji mdogo wa peramiho,na lengo kubwa ni kuwa na
kikosi imara ambacho kitawawezesha kupanda daraja msimu huu.
“maji maji tunaitaji kupanda daraja vyovyote itakavyokuwa
tumesajili wachezaji 6,na bado tupo mawindoni kuwanasa wachezaji wengine
wakubwa kutoka katika vilabu vikubwa hapa nchini,tunaomba wanaruvuma wote
watuunge mkono,alisema mvula.
Mabingwa hao mara 3 wa kombe la muungano walianza kuyumba
toka miaka ya 2000 ambapo adi kufikia hii leo wameshingwa kuimili mikikimikiki
licha ya kupanda ligi kuu mara kadhaa.
Chapisha Maoni