Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Mbwana Makata.



MBWANA makata ni miongoni mwa mlinda mlango bora ambaye alifanikiwa kutikisa soka la Tanzania miaka ya 1985-92 hapa nchini akiwa na club ya Tukuyu stars na Yanga ya jijini Dar es salam.

Makata ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto 7,alizaliwa mwaka 1933,katika kijiji cha makolora mkoani Tanga,wiki hii amekutana na JELAMBA VIWANJANI na kifanya maojiano maalum,na kuelezea kuhusu maisha yake ya soka.

“Nilianza kucheza mpira tangu nilipokuwa shule ya msingi Makolola,Mkoania Tanga,na nilipata nafasi ya kushirika mashindano mbali mbali licha ya umri wangu kuwa mdogo,lakini nilianza kucheza soka la ushindani mwaka 1981 nikiwa na Reli ya Iringa hapo ndipo kipaji changu kilipoanza kuvuma kwa kuwa nilidumu nao kwa kipindi cha miaka 3  na 1984 uongozi wa timu ya waziri mkuu ya dodoma wakanisajili na nilicheza katika kikosi chao nikiwa kama golikipa namba 1,na tukafanikisha kuifikisha mbali timu hiyo.

“Kutokana na uwezo wangu wa kujituma na kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu pindi niwapo langoni,mwaka 86,nikanyemelewa na Tukuyu Stars ya Mbeya,timu ambayo niliichezea kwa mafanikio makubwa sana kwa kuwa kupitia tukuyu stars uwezo wangu wa kucheza soka ulijulikana hadi nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na tukuyu stars ilipata nafasi ya kushirki michuano ya kimataifa yeye akiwa kama golikipa namba 1,mara baada ya timu hiyo kufanikiwa kulitikisa soka la Tanzania kwa kutwa ubingwa mwaka 1986.

“Hata hivyo nafasi yangu ya kubaki tukuyu stars ilififia kwa kasi sana kutokana na timu ya soka ya Yang Africans toka jijini Dar es salam kunisaka kwa udi na uvumba licha ya kwamba timu hiyo ilikuwa na magolikipa mahili sana hapa nchini ikilinganishwa na timu zingine na mnamo mwaka 1988 nikajiunga rasmi na Yanga.

“Nikiwa Yanga nilipata upizani mkubwa sana toka kwa Joseph Fungu na Juma Pondamali ambao kwa hakika walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kulinda lango lakini nilicheza kwa kujiamini huku nikifanya mazoezi mara kwa mara na mwisho wa siku tukawa tunapokezana Kucheza katika mechi mbali mbali za ndani na Kimataifa.

Kuondoka Yanga

“Kipindi kile club zilikuwa hazitulipi mshahara tulikuwa tunapata posho,ila zilikuwa zinamtafutia ajira mchezaji,mimi nilitafutiwa ajira City council,kakini kuna lidandasi lilitokea mwaka 1992,hali ambayo ilipelekea kupunguza wafanyakazi na moja ya watu ambao walikumbwa na zahama hiyo ni Sisi wachezaji ambao tulikuwa tunafanya kazi katika eneo lile kiukweli baada ya tukio lile maisha yangu ya soka yalikuwa magumu sana ndani ya yanga.

“Na hasa hukizingatia tukio lile lilikuwa limetokea muda mfupi mara baada ya kurejea toka kwenye maumivu mazito ya enka,ambayo yalinifanya nisipate nafasi ya kucheza mara kwa mara, nilikuwa nikitegemea posho ambayo ilikuwa haikidhi maitaji yangu,na kipindi kile tulikuwa tunapata posho kubwa katika mechi za Simba na Yanga ambapo tulikuwa tunachukua elfu 19 adi 20,lakini kwa mechi za kawaida tulikuwa tunachukua elfu 3 au 4.

“Sikufanya ajizi kwa usalam wa maisha yangu mwaka 1992 nikajiunga na Rtc Kagera timu ambayo ilinihaidi kunipa ajira ya kudumu,hata hivyo mambo yalienda kombo mnamo mwaka 1993 nikaamua kutundika Daruga na ukawa mwisho wa maisha yangu ya kucheza soka.


“Mwaka 1993-1998,niambua kuachana kabisa na mambo yanayohusu soka nikaamua kujikita katika biashara ili kujijenga kiuchumi,nilikuwa nikisafirisha bidhaa kama vile vipodozi,viatu, sukari na vitu vingine vingi katika maeneo mbali mbali,na nilifanikiwa kuiingizia kipato kikubwa na nikawa naishishi vizuri na familia yangu,lakini mwaka 1998 baadhi ya viongozi na wadau mahili wa soka wakanishauri kujiunga na mafunzo ya ukocha kutokana na mchango mkubwa ambao niliutoa kwa taifa pindi nilipokuwa mchezaji.

“Nililidhia kwa moyo mmoja na  nilifanikiwa kupata mafunzo ya ukocha ambapo timu yangu ya kwanza kufundisha ilikuwa ni Mji Mwapwa ya Dodoma ambayo niliipandisha hadi ligi kuu bara na nikadumu nayo kwa misimu 3 na mwaka 2000 nikajiunga na timu ya Idd Azan mweshimiwa mbunge ambayo nilidumu nayo kwa kipindi cha miaka 4,na timu hiyo ikauzwa na ikafahamika kwa jina la Pan Afrika,na mwaka 2004 nikaamu kuondoka kwa kuwa timu hiyo ilikuwa imeshapata kocha mwingine.

“Safari yangu ya ukocha ilizidi kuwa ndefu na mwaka 2004  nilipata nafasi ya ukatibu mkuu wa kamati ya ufundi ndani ya chama cha soka cha kinodoni,ambapo nikiwa hapo nilifundisha timu ya Copa coca cola ya kinondoni chini ya umri wa miaka 17,na nikafanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

“Kikosi changu cha chini ya umri wa miaka 17 cha kinondoni kimetoa wachezaji wengi sana wenye uwezo wa kusakata kabumbu hapa nchini kwa sasa akiwemo chiritoph Edwald[simba] na Tino Agostino [prisons] ambao wanafavya vyema kwa sasa katika soka la Tanzania,

“Lakini pia mwaka 2008,nilipata nafasi ya kuwa kucha wa mkoa wa kisoka wa Kinondoni katika michuano ya Taifa Cup,ambapo sisi kidondoni tulifanya vizuri sana katika michuano ile na tulikuja kutolewa na wezetu wa Ilala timu ambayo ilikuwa na wachezaji wengi wa ligi kuu akiwemo Musa Hasani Mgosi na Mohamed kijuso,chini ya kocha mwezangu Jamhuri kiweru na wakatawazwa mabingwa.

“Sikuishia hapo baada ya michuano ya Taifa cup kumalizika nilijiunga na wanakishamapanda Toto Afrika ya Mwanza ambayo niliifundisha kwa mafanikio makubwa ikilinganishwa na mwenendo wa timu hiyo kwa misimu mingine lakini mimi niliifikisha nafasi ya Tano ya ligi kuu ya vodacom Tanzania,lakini nikiwa bado niko Mwanza nilipata nafasi ya kuifundisha timu ya mkoa wa mwanza mwaka 2009,tukafanikiwa kushika nafasi ya Tatu,na hapo nikaondoka Mwanza nikajiunga Tanzania prisons ya Mbeya.


“Prisons nilifundisha kwa kipindi cha msimu mmoja na baadae nikaachana nao na nikapata nafasi ya kuchukua kombe la Taifa cup nikiwa na timu ya mkoa wa Mbeya,Mbeya I mwaka 2011 hapo ndipo Nikachukua jukumu la kuonpdoka mbeya na kujiunga na Jkt Oljoro baadae nikajiunga na jkt Ruvu.itaendelea…………….
Endelea kufuatilia kesho tarehe 16 atafafanua kuhusu ushirikina viwanjani.



Chapisha Maoni