Niliishi
maisha magumu Msimbazi mara bada ya kukosa bao la wazi dakika za mwisho mechi
ya kimataifa dhidi ya timu toka msumbiji CCM Kirumba Mwanza. kwa wachezaji
tulionao hivi sasa na mfumo wa uendeshaji wa timu ya taifa, hata kama atashuka
Yesu kushiriki kombe la dunia ni ndoto.
MBUI YONDANI.
Mbui Yondani ni miongoni mwa
washambuliaji wapiga mashuti hatari sana ambao waliwahi tokea hapa nchini na
kamwe hawezi kusahaurika kwa mashabiki na wadau wa soka hapa nchini hasa kwa
Timu ambayo zamani ilikuwa kiboko ya vigogo hapa nchini nazunguzia Reli
Morogoro .
Yondani ambaye ni mzaliwa wa
mtaa wa Kirumba Polisi Jijini Mwanza ambaye ni Baba yake mdogo wa Beki
mahili wa Yanga Kelvin Yondani, alianza kusakata kabumbu wakati akiwa mdogo
katika shule ya Msingi mwenge iliyopo Jijini Humo.
Katika Mazungumzo maalum na
JELAMBA VIWANJANI ameeleza kwa kina kuhusu historia yake ya soka;
“Licha ya kucheza mpira katika
timu ya Uwanja CCM Kirumba pamoja na Basuko,nilianza kucheza soka la ushindani
mwaka 1988 katika timu ya Copy United ambayo ni timu ya watoto wa mjini Mwanza
timu ambayo wamepitia wanasoka wengi wa mkoani Mwanza.
“Mwaka 1989 nilijiunga na Reli
ya Morogoro timu ambayo ilikuwa tishio kwa vigogo hapa nchini nazungumzia Simba
na Yanga,wakati nipo Reli nilipata nafasi ya kuchezea timu ya Taifa kwa mara ya
kwanza mwaka 1992 kutokana na kiwango changu kuwa juu sana kwa kipindi
hicho,nakumbuka tulicheza kwenye michuano ya Challenge ambapo Tanzania
tuliwakilishwa na Kaka Kuona pamoja na Victoria,Hayo ni majina ya timu ya Taifa
Sisi tuliwakilishwa na timu mbili kwa kuwa tulikuwa waandaaji .
“Baada ya kupata nafasi ya
kuitumikia Timu ya Taifa mwaka 1993 nikasajiliwa na Simba ya Jijini Dar
Es Salam,Timu ambayo niliichezea kwa msimu mmoja lakini kutokana na mizengwe,kocha
alikuwa anawapanga wachezaji kulingana na mapenzi yake hata kama wewe ni
mzuri,Na ni ukweli usiopingika kipindi kile nilikuwa mchezaji wa kiwango
cha juu sana,
“Baada ya kuona kwamba Simba
naweza nikaua kiwango changu mwaka 1994 nikatimukia Milambo ya
Tabora,lakini kutokana na maisha magumu ya huko Tabora,Timu yangu ya Zamani
Reli ya Morogoro wakaamua kunirudisha, hapo nilicheza kwa miaka miwili 1996
hadi 1998.
“Mwaka 1998 hapo nilifikia juu ya
kustaafu soka na kuangaika kuhusu
maisha yangu kwa kuwa kwa kipindi chote hicho sikuwa vizuri kiuchumi, nikaacha
kucheza Soka la ushindani nikachezea Mwanza Veterani Pamoja na Pamba ya mwanza
ambapo Mwaka 2002 nikaacha kabisa kujihusisha na Mambo ya soka hapo ndipo
nikatundika Daruga Rasmi.
Nakumbuka.
“mwaka 1990 wakati nipo Reli ya
Morogoro tulicheza na Timu ya soka ya Maji Maji ya Songea,katika pambano hilo
ambalo lilikuwa kali sana kutokana na Maji Maji kuwa na kikosi imara hadi
kipindi cha kwanza kilipomalizika nakumbuka tulifungana bao 1-1,
“Kipindi cha pili mchezo ulianza kwa
kasi sana ambapo dakika za mwisho nilipokea Pasi safi nje ya 18 na bila kufanya
ajizi nilifumua Shuti kali ambalo lilipeleke mlinda mlango wa Maji Maji
kuchanika mikono na kuachia mpira ukaingia Wavuni.
“Mimi mwenyewe nilishangaa sana
tukio lile mara baada ya kumkuta bwana Shaibu Kambanga Disko usiku baada ya
mechi akiwa amefungwa bendeji,nikampa pole na akanieleza kuwa hakuwai pata
mkwaju kama ule,tukaendelea kuburudika.
“Nakikumbuka kikosi cha Reli ambacho
kilikuwa kiboko ya Vigogo na Timu zingine hapa nchini,ambacho akitakuja
sahaurika hapa nchini ambapo langoni alikuwepo Athumani Msumari,safu ya ulinzi
iliimalishwa na James Charles[marehemu],Abdallah
Mkali[marehemu],Gasper Lupindo[marehemu] pamoja na Fikiri Magoso. Viungo
alikuwepo Mtwah Kiwelu,Boniface Njohore pamoja na Dankani Butinini huku safu ya
ushambuliaji ikiongozwa na mimi mwenyewe Mbui Yondani,Msafiri Khamis Bila
kumsahau Living Stone.
Hawaezi kusahau
“Mwaka 1991 mechi ya ligi kuu kati
ya Reli na Bandari ya Mtwara mimi na beki wa Bandari tuliruka juu kuuania mpira
mara baada ya kuingizwa majaro zuri toka winga ya kulia bahati mbaya tukaukosa
mpira na tukagongana Vichwa na tukadondoka vibaya sana.
“Katika tukio lile mwenzangu alipata
fahamu baada ya siku ya Tatu,mimi japokuwa nilirudi uwanjani kuendelea na
mchezo usiku uliofuata sikupata usingizi nilipata maumivu ambayo sikuwai kuyapata
tangu nilipozaliwa kwa Baba na Mama, ambapo baada ya siku chache niliendelea na
mchezo.
Endelea kusoma
jelamba viwanjani sehemu ya pili atasimulia kuhusu imani za kishirikina pamoja
kubebeshwa gunia la misumari na samba usikose.
Chapisha Maoni