ENDELEA KUFUATILIA HISTORIA YA MBUYI YONDANI BABA MDOGO NA KELVIN YONDANI MCHEZAJI WA SASA WA YANGA.
ILIPOISHIA JANA……………………..
“Mwaka 1991 mechi ya ligi kuu kati
ya Reli na Bandari ya Mtwara mimi na beki wa Bandari tuliruka juu kuuania mpira
mara baada ya kuingizwa majaro zuri toka winga ya kulia bahati mbaya tukaukosa
mpira na tukagongana Vichwa na tukadondoka vibaya sana.
“Katika tukio lile mwenzangu alipata
fahamu baada ya siku ya Tatu,mimi japokuwa nilirudi uwanjani kuendelea na
mchezo usiku uliofuata sikupata usingizi nilipata maumivu ambayo sikuwai kuyapata
tangu nilipozaliwa kwa Baba na Mama, ambapo baada ya siku chache niliendelea na
mchezo.
ENDELEA………………
Ushirikina
“Upo hasa kwa virabu vikubwa Simba
na Yanga mara nyingi hasa katika mechi za watani wa jadi lakini kwa timu
zingine kama Reli sikushuhudia suala lolote la ushirikina tulikuwa tunafanya
mazoezi na kumtegemea mungu.
“Siamini hata kido imani hizo sio
kweli ,wakati nipo Simba kuna mambo mengi yalikuwa yanafanyika wakati wa
mchezo lakini tulikuwa tukichezea kichapo kama kawaida.
Simba walinibebesha Gunia la
Misumari.
“Mwaka 1993 wakati nikiwa
Simba,nilikosa bao Ya wazi wakati zikiwa zimesalia dakika 3 mpira
kumalizika,katika kombe la Caf kwa sasa shirikisho,kati ya Simba na Timu Toka
Msumbiji,nakumbuka ilikuwa CCM Kirumba Mwanza mchezo ambao ulimalizika kwa sare
ya bila kufungana.
“Baada ya mechi ile sikuwa na
amani,wenye timu walinitazana kwa jicho baya huku wakinituhumu kuwa mimi
ni mpenzi wa Yanga na kwamakusudi nikaamua kuwakosesha Simba ushindi kiukweli
iliniuma sana.
“Basi kutokana na tuuma ile na licha
ya kwamba kiwango changu kilikuwa kikubwa masikini ya mungu sikupewa nafasi
hata ya kusafiri na timu kwenda nchini Msumbiji katika mechi ya marudiano
waliniacha Bongo.
“Kuanzi hapo nilichukiwa sana hadi
nikhathirika kisaikorojia pindi nikiwapo uwanjani lakini ukweli ni kwamba mimi
sikuwa na mapenzi na Yanga na kukosa Bao ni suala la kawaida kwa mchezaji sio
makusudi.
Endelea
kusoma jelamba viwanjani sehemu ya tatu kuhusu waamuzi,katiba na kipa ambaye alimsumua sana usikose.
Chapisha Maoni