Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
 
Timu ya kimondo Sc ya mkoani hapa inayoshiriki ligi daraja la kwanza imeiadhibu timu ya Real Northerdg ya nchini Zambia kwa kuifunga  goli 2-1 katika mchezo wakirafiki ulio chezwa  katika uwanja wa nakonde nchini humo.
 
Timu hiyo ambayo inashiriki ligi dalaja la kwanza nchini Zambia ambapo nimoja ya maandalizi kwa  timu ya Kimondo kwajili ya msimu mpya wa ligi , timu hiyo kwasasa inanolewa na kocha  Habib Kondo akisaidiwa na Anton Mwamlima.
 
Mchezo huo ambao ulianza kwa  timu ya Kimondo kutamba uwanjani hapo  huku wenyeji wao wakihaha kama wako katika uwanja wa ugenini.
 
Timu ya kimondo ndiyo ilikuwa yakwanza kuliona lango la wapinzani wao katika dakika ya 15 kupitia kwa mchezaji wake  mahili Athuman Ally  wakati goli lapili lilitiwa kimyani na Asifiwe Lwinga dakika ya 66 baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa timu pinzani.
 
Timu ya Real Northerdg   ilifanya mashambulizi lakini yaliishia jiani hayakuweza kufika katika   lango la wapinzani wao  kutokana na  mabeki wa timu pinzai kuilinda vema ngome yao.
 
 
Dakika ya 85  wachezaji wa Kimondo Sc walijisahau ambapo wapinzani wao walitumia nafasi hiyo nakufanya mashambulizi ambayo yalizaa  matunda  ya kupata goli hilo la kufutia machozi lililo fugwa na  James Sinkala.
 
Hadi mchezo huo unamalizika Real Northerdg   ilikuwa imeshindwa kuutendea haki wanja wao wa nyumbani kwa kukubari kipigo cha goli 2-1.


Chapisha Maoni