Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Michuano ya kupambana na ujangili wa wanyama pori katika hifadhi ya ruaha, Spanet cup yanayoendelea katika tarafa ya Idodi pamoja na Pawaga yamefikia katika hatua ya nusu fainali michezo ambayo itafanyika jumamosi na jumapili mwishoni mwa wiki hii. 

Mashindano hayo yenye rengo la kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuwatunza wanyama pori hasa tembo ambao wanatoweka kwa wingi, timu ambazo zitaonyeshana kazi wikendi hii ni pamoja na  Tunundu FC watavaana na kitisi siku ya jumamosi huku Idodi watapepetana na Kijika siku ya jumapili ambapo timu zitakazofuzu zitakutana katika fainali.

Akizungumzia michuano hiyo mratibu wa mashindano Godwell Oleneng’ataki Alisema kuwa baada ya mashindano hayo timu zitajinyakulia zawadi mbali mbali pia bingwa wa michuano atapewa nafsi ya kutembelea hifadhi ya Ruaha  na kuandaaliwa pambano na timu ambayo itatajwa hapo baadae.

Michuano hiyo itasaidia pia kuibua vipaji toka kule vijijini ambako kuna wachezaji wengi wazuri lakini bado hawajapata nafsi ya kuonyesha uwezo wao na badala yake wanajiingiza katika suala la ujangili.


Chapisha Maoni