Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 

 

 

Na Boniface Wambura

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora (pichani chini).
Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).

Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.

WAKATI huo huo
YANGA SC wametakiwa kuwasilisha jina la kocha wao mpya, Mbrazil Marcio Maximo na wasaidizi wake.
Hiyo imo katika agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuzitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha orodha ya watendaji wa mabenchi yao ya ufundi yakiongozwa na Kocha Mkuu.
Ni wajibu wa klabu kuhakikisha zinatekeleza maagizo hayo kwani ni matakwa ya Kanuni za VPL na zile za FDL.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu wakati ile ya FDL inatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.


Chapisha Maoni