Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




BAADA ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kutolewa na Msumbiji katika mchezo ambao ulifanyika nchini msumbiji kwa Stars kuchabangwa bao 2-1 baadhi ya wadau toka mkoani Iringa wamesema wakati wa stars kuachana na kutoa sababu zisizokuwa za lazima pindi watolewapo katika michuano mbali mbali umeshafika.
 16
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa katika nyakati tofauti wadau hao walisema TFF ikae chini na kuandaa mipango ya muda mrefu ikiwemo kuwekeza kwa vijana wadogo na kujenga miundombinu ya soka suala ambalo litapelekea timu ya taifa kucheza vizuri tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hakuna ligi za vijana za kuaminika.
“kuna baadhi ya wachezaji wameachwa ambao ni wazuri ambao wanaweza kutusaidia,tuwachukue wachezaji wazuri, pia soka la vijana tumelifumbia macho ndio soka ambalo ni msaada kwa timu mbali mbali duniani tusipokuwa makini tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu,alisema Antoni mgata.
Kwa upande wake Issa Langu alisema kuwa timu yetu mara nyingi imekuwa ikifanya maandalizi ya zima moto suala ambalo litatuwia vigumu kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa michuano ambayo mara nyingi tunakutana na timu ambazo zinakuwa zimejiandaa Zaidi yetu.
Stars imetupwa nje ya mashindano mara baada ya kufungwa bao 2-1 dhini ya msumbiji katika mchezo uliopigwa pale nchini msumbiji ambapo mchezo wa kwanza ambapo ulifanyika katika uwanja wa taifa wa Dar es salamu timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2.


Chapisha Maoni