Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Timu ya Mbeya City ilismamisha shughuli za mji wa tunduma kwa muda   mkoani Mbeya  baada ya kuingia katika mitaa ya mji huo ilipokuwa ikienda kucheza mechi ya kirafiki Nchini Zambia juzi.



Mashabiki hao ambao waliipokea timu hiyo  kutoka kijiji cha Mpemba  kabla aija fika Tunduma wakiwa wamepanda Trekta  na wameva jezi za timu hiyo  huku pikipiki zikipeperusha bendera.

Baada ya kuingia Tunduma mamia ya washabiki waliokuwa wakifanya biasha zao katika  mji huo waliacha shuguli zao nakuja barabarani  kuwashangilia wachezaji wao  hali ambayo iliwalazimu madereva kupunguza mwendo ili mashabiki hao wawasalimi wachezaji.

Mashabiki hao ambao walijikuta wamegeuka kuwa askari wa barabarani baada ya kufika mpaka wa kuingia  nchini Zambia  kukuta foreni kubwa  nakuanza kuliongoza gali la wechezaji nawakati mwingine kuwalazimu kwenda kuwaomba madereva wa malori walipishe basi hilo huku wakiwambia wapisheni wanaume wakachinje  Zambia.

Mashabiki wa Tanzania walienda Nchini Zambia kwa mchakamchaka hadi uwanja  wa nakonde ambapo mchezo kati ya Mbeya City na Combine ya Zambia ulipo chezewa na kurudi kwa kishindo baada ya kutoka na ushindi wa goli 1-0.


Vile vile Wadau wa soka wa Tanzania wamekilalamikia chama cha mpira cha Zambia kuwa hawana utaratibu mzuri wa kuandaa michezo  baada ya kuanza kuuza tiketi  za mechi ya Mbeya City na Combine ya Zambia  baada ya timu kuingia uwanjani hali iliyo leta vurugu kubwa getini.

Mchezo huo wa Mbeya City dhidi ya Combine ya Zambia  ulichezwa katika uwanja wa Nakonde  ulizua balaa baada ya  tiketi hizo kuanza  kuzwa  mara baada ya timu  kuingia uwanjani na kusababisha msongamano mkubwa  kwa wauza tiketi na katika geti la kuingilia.
Wakiongea na cjelamba viwanja  Ally Shombe alisema kuwa  watu wa huku huwa hawaezi kuingia uwanjani kabla timu haijafika lakini kwa leo wangeanza kuuza tiketi mapema  kwani  sisi watanzania huwa tunaingia uwanjani mapema siyo kama wao.
“Ona saiza  tunavyo  pata shida ya kupata  tiketi na kuingia kutokana na uwingi wa mashabiki  kutoka Tanzania na Zambia  mashabiki watu bado,  wengi bado hatujapata tiketi sijui kama tutaingia uwanjani, mpira umeisha ona hadi watu wana pigwa virungu  na maskari  kutokana na utaratibu wao mbovu “

“tiketi zingeanza kuuzwa toka asubuhi,  Mbeya City   sisi kwetu nitimu kubwa  timu yetu ya nyumbani kwa hiyo uwanja wowote itakapocheza sisi mashabiki wao tupo nyuma .


Kwani hata mpira ulipo malizika mashabiki wengi hawakutokea getini walionekana wakiruka ukuta ilikutoka kutokana na uwingi wa mashabiki waliyo kuwa uwanjani hapo na mrango wao ni mdogo.


 LIGI DARAJA LA KWANZA MBEYA CITY NA BURKINA FC JAMHURI MORO PIX NO 1

Katika hali nyingine ya kushangaza baada ya mpira kupigwa kutoka nje ya uwanja  haukurudi baada ya watu walio kuwa nje kutokomea nao  mpira ,huku wenyeji wakisema upande huo mpira ukitoka nje huwa unaibiwa ni upande wa maghalibi mwa uwanja.



Chapisha Maoni