Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Muhamed Kijuso



Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
 
Mchezaji mkongwe wa Mbeya City  Muhamed Kijuso akabidhiwa  ukocha timu ya U20 katika timu yake ya Mbeya City  inayo shiriki ligi kuu.
 
 
Mchezaji huyo ambaye aliitumikia timu hiyo kwa mda mrefu na hadi msimu uliyo pita alikuwa bado akiitumikia timu yake  na msimu huu kaachana na mikiki mikiki ya soka na kutulia katika benchi la ufundi katika timu ya U20.
 
 
 Akimtambulisha kwa mashabiki wa tawi la Tundu mwenyekiti wa timu ya Mbeya City Musa Mapunda alisema kuwa   tumeamua kumuweka kijuso katika bechi la ufundi ambapo atakuwa akishughulika na vijana wa U20  hasa pale mwalimu msaidizi wa timu mkubwa anapo kuwa yupo safarini na timu.
 
“Lengo letu kubwa nikupata kikosi kizuri zaidi cha U20 ambacho kitatusaidia kuwa  na wachezaji wengi ambao tutakuwa tumewaanda sisi wenyewe  na watakao kuwa wamesha zoea mazingira  yetu na siyo kuwasajiri wageni”
 
“Ninaimani kubwa sana baada ya mda tutakuwa na wachezaji wengi na wenye uwezo kutokana na timu ya U20  kupata walimu  wazuri na wenye uzoefu akiwemo Kijuso”
 


Chapisha Maoni