Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





ALIYEKUWA katibu mkuu wa chama cha soka cha Iringa God Mvela amesema mpira ya mkoa wa Iringa unakabiliwa na matatizo mengi ambayo kama Hayatatafutiwa ufumbuzi itapelekea iringa kuendelea kudumaa katika mpira wa miguu.

Akizungumza na chanzo Mvela alisema moja ya matatizo makubwa ambayo yameonekana kuwa kikwazo ni pamoja na Tatizo la maamuzi uwanjani,wadau wa soka Iringa kutokuwa Tayari kuchangia mpira,majukumu ya mpira kuachiwa chama cha soka pekee yake pamoja na matatizo ya viwanja.

“ni tatizo sana mimi nikiwa madarakani nilijitaidi kupigana sana ikiwemo kutoa kozi za waamuzi, kozi chache za makocha pamoja na kuandaa viwanja lakini bado inakuwa ngumu kwa kuwa mpira ni Fedha suala ambalo tulikuwa tukiachiwa viongozi pekee yetu ni tatizo sana mabadiliko lazima yawepo katika soka la Iringa.

Pia aliongeza kwa sasa duniani kote mpira unaitaji uwekezaji mkubwa ambapo serikali inatakiwa kutoa Ruzuku kwa vyama vya michezo kama inavyotoa kwenye vyama vya siasa kwa kuwa bila michezo ni ngumu sana kufika mbali kimaendeleo na kufahamika duniani.

Kwa sasa kuna timu mbili ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza ambazo zinapigana ili kuhakikisha zinapanda ligi kuu ambapo kwa takribani miaka kumi na 14 sasa mkoa wa Iringa hauna timu ya ligi kuu.


Chapisha Maoni