Shirikiso la soka barani Afrika limeikabidhi
Cameroon, jukumu la kuandaa Afcon 2019, katika kikao cha kamati kuu ya CAF
kilichofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kamati hiyo iliamua pia kuipa Ivory
Coast wajibu wa kuandaa makala ya mwaka wa 2021.
Hata hivyo CAF ilitangaza kuwa
Guinea ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa makala ya 2023 kinyume na matarajio ya
wengi.
CAF iliamua kuwatunuku Guinea
uwenyeji wa mashindano hayo kabla ya kukamilika kwa muda uliowekwa kwani Guinea
ilikuwa imeonesha ari na hamu ya kuandaa makala hayo jambo ambalo liliisaidia
kuzipiku Algeria na Zambia ambazo zilikuwa zinawania uwenyeji huo.
Cameroon, itakuwa inaandaa makala
hayo kwa mara ya pili baada ya kuwa mwenyeji wa makala ya 1972 ya mashindano
hayo ya Afrika.
Kulingana na taarifa ya CAF
,Cameroon,inalenga kutumia viwanja vya Bafoussam, Douala, Garoua na Yaounde
kufanikisha awamu hiyo ya mashindano.
Furaha hiyo ya kutuzwa kuwa wenyeji
wa mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika ilitanda hadi Ivory Coast, ambayo
imeratibiwa kuandaa makala ya mwaka wa 2021.
Hii vilevile itakuwa mara ya pili
kwa taifa hilo kuwa mwenyeji wa mchuano huo baada ya kuandaa kipute cha mwaka
wa 1984.
Ivory Coast imeratibu kuandaa
mashindano hayo katika miji ya Abidjan, Bouake, Korhogo, San Pedro na mji mkuu
wa Yamoussoukro.
AFCON :Ivory Coast kuandaa
2021,Guinea 2013
Guinea haijawahi kuandaa mashindano
haya katika historia yake ya miaka 57.
Makala ya kwanza ya kombe la mataifa
bingwa Afrika yaliandaliwa katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.
Katika ombi lao kamati andalizi ya
Guinea inapanga kuandaa mashindano hayo katika miji ya Conakry, Kankan, Labe na
Nzerekore .
Sadfa ni kwamba CAF imeipiga
marufuku Guinea kutoandaa mashindano yeyote kwani taifa hilo limeathirika na
mlipuko wa Ebola.
Zambia licha ya kuwa ilishindwa
ilikuwa imepanga kuandaa mashindano hayo katika ukanda wa ziwa Victoria.
Hiyo ndiyo mara ya pili kwa Zambia kupoteza
nafasi ya kuandaa mashindano ya Afrika baada ya kupokonywa uwenyeji wa mwaka wa
1988 iliposhindwa kuthibitisha uwezo wake kwa wakati ufaao.
Makala ya mwaka huo yaliandaliwa na
Morocco.
Kwa upande wao Algeria walitongewa
na kifo cha mshambulizi wa JS Kabylie kutoka Cameroon Albert Ebosse baada ya
kugongwa na jiwe akiwa uwanjani .
Kenya, Algeria, Ethiopia, Ghana,
Mali na Zimbabwe zinawania kuandaa makala ya 2017 baada ya Libya kujiondoa
kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi
ni Septemba 30.
by bbc
Chapisha Maoni