Klabu ya Algeria JS Kabylie imepigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote kwa miaka miwili.
Shirikisho
la soka la barani Afrika CAF limefikia kauli hiyo baada ya kuuawa kwa
mshambulizi wa Cameroon Albert Ebosse uwanjani mwezi uliopita.Ebosse alikufa baada ya kupurwa na jiwe baada ya mechi ya ligi kuu ya Algeria.
Marufuku hiyo inatarajiwa kuathiri pakubwa Kabylie ambayo ilikuwa imefuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita.
Caf vilevile imeratibua kuanzisha tuzo kwa heshima yake Ebosse.
Klabu hiyo tayari imepigwa marufuku ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wote wa 2014-2015 .
Aidha mashabiki wake hawawezi kushuhudia mechi yake yeyote nyumbani wala ugenini.
BY BBC
Chapisha Maoni