Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


ALEX MAPUNDA MWANDISHI



Omari Husein
Omari Husein ni miongoni mwa walinzi imara kabisa kuwai kutokea hapa nchini na  timu ya Maji Maji ya Songea ambaye kamwe awezi kusahaulika kwenye orodha ya wachezaji ambao watakumbukwa katika tathinia ya soka milele hasa kwa wadau na wapenzi wa timu ya Maji Maji.

  Husein mzaliwa wa Kata ya Ligula Mtwala alianza kucheza soka katika shule ya msingi Karume Newala huko Mtwara na kufanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa hali ambayo ilikuw gumzo kubwa shuleni hapo na maeneo ya jilani ya Newala, katika Mazungumzo Maalum na Championi anafafanua Mengi kuhusu Maisha yake ya soka.

  ''Nilianza kucheza soka la ushindani nikiwa na Bandari ya Mtwara mwaka 1987 timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la pili na nilicheza hapo kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo mwaka 1990 nilijiunga na Maji Maji ya Songea baada ya wao kuridhika na uwezo wangu.

  ''nilicheza Maji Maji kwa kwa kipindi cha miaka 9 ilikuwa panga upangue lazima mimi niwepo kwenye kikosi cha kwanza hali ambyo ilipelekea vigogo wa soka hapa nchini kuingia kwenye mapambano ya kusaka saini yangu.

  ''lakini mwaka 1999 nikajiunga na Wekundu wa Msimbazi simba timu ambayo niliichezea kwa Misimu miwili na kutokana na fitina za msimbazi mwaka 2001 nikarudi kuitumikia Maji Maji ya Songea kwa mara ya pili.

   ''Niliichezea timu yangu kwa moyo wote ambapo mwaka 2005 nikajiunga na timu ya Jeshi la Wananchi {FFKJ} toka Mbeya ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kuu lakini mwa 2006 nikarudi kumalizia soka langu kwa mara ya tatu katika timu ya Maji Mji Sc na mwanzoni mwa mwaka 2007 nikasitaafu rasmi kusakata kandanda,anaeleza Omari Kisha anaendelea.


  Simba,Yanga walinigombanisha na Baba mzazi.

  ''Mwaka 1999 ulitokea ugomvi mkububwa kati yangu na  Baba  Mzazi kisa alitaka nijiunge na Yanga kwa pesa kidogo kwa kuwa yeye ni Mwanachama wa Yanga mwenye Kadi,suala ambalo liliniweka katika mazingira magumu  sana kwa kuwa Simba walikuwa wamehaidi dau nono kuliko Yanga  na ukizingatia mimi binafsi katika familia ya mzee Daima nilikuwa na Mapenzi na Simba.
  ''niliamua kukaa chini na Mzee na kumwelekeza vizuri kuhusu safari yangu kwenda Simba na mapatano ambayo mimi na Simba tulifikia na mzee alikubari japo kuwa kwa shingo upande akanirusu kwenda  simba.

Ubinafsi uliniondoa Simba.

  ''Timu zetu zinazojiita timu kubwa kuna ubabaishaji mkubwa wa usajili kwa kuwa kila kiongozi anataka kuingiza watu wake anaowataka kwa mapenzi yake.

  ''Mimi wakati natoka Maji Maji kwenda Simba uwezo wangu wa kusakata kandanda kama beki ulikuwa juu sana lakini baada ya kutua Simba wakanifanyia fitina baadae nikawa nasugua benchi na wakawa wanawapanga wachezaji wanaowajua wao ambao nilikuwa nimewazidi kiwango na baada ya kukaa muda mrefu morali ya kucheza mpira ikapungua lakini ilipofika wakati wa usajili nikasikia taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa wameamua kuniacha kutokana na kushuka kwa kiwango changu.

  ''Kauli ile ilinishitua sana kutokana na thamani ya uwezo wangu kuwa juu,sikuwa na jinsi niliamua kurudi timu yangu ya Maji Maji timu ambayo niliichezea kwa kiwango cha hali ya juu sana kama ilivyokuwa mwanzo.

Siku ya kwanza kupanda ndege nilitetemekatetemeka sana.  

  ''Nakumbuka tulienda Misri kuwakirisha nchi katika michuano ya club Bingwa Afrika ambako tulivaana na National Alhily katika mchezo wa marudiano ambapo mechi ya awali walitufyatua bao 3-0 zote zilifungwa na mchezaji mmoja Hossam Hassan mechi ile iliktwa na  mtihani mkubwa kwangu kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kwangu kupanda ndege na wakati tunaelekea uwanja wa ndege ili kuondoka nilitetemeka sana kiasi cha kugairi safari na Akiri yangu ilinituma kuwa usafiri wa ndege ni hatari na nilijua kuwa ni mwisho wa maisha yangu.

  ''Lakini nilipiga moyo konde na tukaingia kwenye ndege kuelekea Misri baada ya kuwasili kairo wenyeji wa kule walitufanyia ujuma ili kutuondoa mchezoni,kwanza walituweka uwanja wa ndege kwa saa zima na baadae wakatupeleka hoteli ambayo haikuwa na hadhi na wakati wa chakula walitupa chakula ambacho sio kizuri kwa wachezaji  
Hali ambayo ilipelekea balozi wetu kutupatia chakula cha mchana kabla ya mchezo kuanza,wakati wa mechi ulipofika nakumbuka tulicheza vizuri sana lakini tulifanya uzembe dakika za mwisho hali ambayo ilimpa nafasi star wa misri Hossam Hassan atuumize kwa mara nyingine ambapo alitushindilia 2-0, bao ambazo zilihitimisha karamu ya yeye kutufumua bao 5-0,na tukaaga mashindano na kurudi Tanzania vichwa chini.

Mashabika wa Simba walivyunja vioo basi la timu letu.

  ''Nakumbuka mwaka 2001 kulikuwepo na pambano la watani wa jadi Simba na yanga mchezo ambao ulifanyika Shamba la Bibi Jijini Dar es salam mchezo ambao Simba tulifungwa bo 2-1 na Yanga mabao yalifungwa na Iddi Moshi Mnyamwezi,pamoja na Fred Mbuna huku la kufutia machozi kwa upande wetu liliwekwa kimiani na Mrisho Moshi.

  ''Baada ya kumalizika kwa pambano hilo mashabiki wetu walilivaa basi letu na kuanza kupiga mawe wakidai kuwa tulifungwa makusudi ili kuwaumiza wao.

  ''Katika tukio lile Golikipa wa Simba mwalami Mohamed aliumizwa ambaye kwa sasa anachezea Macheje ya Msumbiji na baadae Polisi waliingilia kati na kutusindikiza hadi hotelini Kibaha.

  ''Tukio lingine ambalo Lilitokea siku ya mchezo huo ni Mchezaji wa  Simba Wiliam Fani Bula alikosa Penalti kipindi cha pili ambayo ilidakwa kwa umahili mkubwa na  Isimail Suma,
baada ya mchezo kutokana  na hasira ambazo alikuwepo nazo aliamua kurudisha Vifaa vya michezo vya Simba na kuelekea nchini Riberia.

Nilivunjika Mbavu ajali ya Misungwi.

 ''Nakumbuka mwaka 1996 Maji Maji tulikuwa tunatoka kucheza na Pamba ya mwanza mchezo ambao tulishinda bao 2-1,wakati wa kurudi dereva wa basi letu akiwa katika mwendo kasi tulipata ajari katika eneo la Misungwi nje kidogo ya Mji wa Mwanza na katika eneo hilo bara bara ilikuwa inatengenezwa kutokana na mwendo kasi basi likaächa njia na kupinduka na wachezaji wetu wengi muhimu waliumia katika ajali ile na kulazwa bugando.
  ''Katika ajari ile mimi nilivunjika Mbavu,Shaibu Kambanga alikatika sikio,Doi Moke alikatika nyama za paja, Diwa Omari alivunjika kidole,Amburosi alipasuka kichwani na kuvuja damu nyingi sana huku Hali Mapero aliumia goti na kufungwa pio pii ngumu.

  ''siwezi kuisahau ajari ile kwa kuwa tulikaa bila kucheza kwa kipindi cha miezi mitatu na kikubwa tunashukuru mungu baada ya ajali ile hatukuchelewa sana mwanza mkuu wa mkoa kipindi kile Anna Makinda aliwasiliana na mkuu wa Mkoa wa Mwanza na akatupatia usafiria ambao ulituleta adi Songea na tukapata matibabu ya uhakika.

Imani za kishirikina.

  ''Zipo michezoni lakini mimi siamini kama zinaongeza kitu chochote zaidi ya kuleta chachu michezoni,kikubwa katika mpira ni mazoezi na kujituma uwanjani.

 ''Lakini kuna tukio nalikumbuka wakati nipo Simba  mwaka 2001 usiku aliletwa Kondoo kwenye gari na wazee kama wanne hivi walikuwa wamevaa kazu na Kondoa alikuwa amevalishwa Sanda nyeupe,mimi nikamuuliza mchezaji mwezangu kuhusu lile tukio alinishangaa sana akaniuliza wewe ulikotoka huko songea mlikuwa hamfanyi hayo?,sikumjibu nikanyamza baadae wachezaji wote tulimzunguka yule Kondoo huku wakiomba dua zao na asubuhi wakaenda kumfukia yule kondoo Pia nakumbuka tulipewa na matunguli ya kuweka kwenye viatu kama dawa.

   ''Lakini mara baada ya Pambano tulikung'utwa bao 2-1 na wapinzani wetu yanga,hali ambayo ilinifanya nipuuzie imani za kishirikina hadi leo.

Wachezaji anaowapenda.

  ''Kwa ligi ya sasa wapo wachezaji wanaonikosha wakiwa uwanjani ambao baadhi yao ni Kelvin Yondani,Julius Mlope pamoja na Sulum Abubakari {sure Boy}.

Ushauri kwa timu ya Maji Maji.

  ''Jamani mimi kichwa kinauma kuhusu timu yetu lazima tuiunge mkono ili iweze kufanya vizuri,watu wanaicheka Maji Maji wakati hawaichangii,lazima wadau na wapenzi wa soka wa hapa wakumbuke kuwa hata kama wataichukia timu uchanguzi wa viongozi unafanyika kila baada ya miaka 4 hivyo ni vema kuleta mshikamano ili kuendeleza timu yetu na kufikia malengo.

     
Baada ya kustaafu soka.

  ''Kwa sasa nafanya kazi ndogo ndogo za kufuga kuku na Kunyoa pia ni Mkulima lakini ndani ya soka kwa sasa ni Meneja msaidizi wa Maji Maji Sc pia ni kocha ya Matarawe Fc.

''Mungu amenijalia naishi vizuri na Mke wangu pamoja na watoto wangu 4,anahitimisha Omari Husein ambaye timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilimpa kisogo mara baada ya yeye kutojiunga na timu hiyo alipoitwa kwa mara ya kwanza kwa kuwa alikuwa akiitumikia timu yake adhimu ya Maji Maji katika kombe la Muungano dhidi ya  Malindi ya Zanzibar ambapo Maji Maji waliibuka mabingwa mwaka 1998,basi ikawa mara yake ya mwisho kuitwa kwenye timu ya taifa.


Chapisha Maoni