Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Alex Mapunda >mwandishi


RAJABU MTWANGE MDIGO
Miongoni mwa nchi ambazo zimejaaliwa na mwenyezi mungu kuwa na vipaji vya kweli vya soka  ni pamoja na Tanzania nchi  ambayo inapatikana mashariki mwa bara la Afrika,miongoni wachezaji hao wenye vipaji ambao waliwiki hapa nchini miaka ya 1985 hadi 1995 ni Rajabu mtwange mdigo ambaye aling’aa akiwa na timu ya Afrikan wonderous ya Iringa,Tukuyu Stars ya  mbeya  Pamoja na Reli ya morogoro kiboko ya vigogo kipindi hicho.
Mdigo,Mzaliwa wa Iringa huko karenga, alianza kusakata kabumbu akiwa shule ya msingi ambapo alisoma shule nyingi ikiwemo,Irolesi,mafinga pamoja na mwembe togwa shule ambayo alimaliza nayo,na baadae alijiunga na masomo ya sekondari katika shule ya Highland sekondari alikuwa akisoma pamoja na kucheza mpira mtaani.
Mdigo alianza kucheza soka la ushindani akiwa na timu ya Afrikani wanderous mwaka 1988 timu ambayo wamepita wachezaji wengi wakubwa hapa nchini waliotokea katika timu hiyo akiwemo Isihaka majariwa ambapo baada ya nyota yake kung’aa sana akasajiliwa na Tukuyu Stars ya mbeya timu ambayo aliitumikia kuanzia mwaka 1990 hadi 1993 kwa mafanikio makubwa.
Safari yake ya kusakata kandanda iliendelea ambapo safari hii akijiunga na Reli morogoro kiboko ya vigogo  ambayo ilikuwa ni moja ya timu  tishio kwa vigogo simba na yanga lakini kufikia mwaka 1995 akatundika daruga akiwa na Polisi Morogoro,anasimulia Rajabu mdigo kasha anaendelea:-
Sababu za kustaafu mpira mapema.
“kiukweli niliamua kuacha mpira licha ya kuwa na ndoto za kuchezea timu kubwa lakini maumivu ya goti pamoja na hali mbaya ya maisha,unajua mpira wa kipindi kile tulicheza kwa kutumia vipaji ambavyo tulikuwanavyo lakini kwa upande wa maisha hali ilikuwa ngumu kwa vile ilitulazimu kucheza mpira pamoja na kufanya shughuli zingine ili kujikimu kimaisha.
“ndio maana wachezaji wengi ambao tulicheza zamani hatuna maisha mazuri ukitulinganisha na wachezaji ambao wanacheza sasa ivi ambao wamefanikiwa kupitia soka.
Siwezi kusahau kifo cha mlinda mlango wetu
“kila nikikumbuka tukio hilo naishiwa nguvu kwa kuwa mwezetu alikufa kwa sababu ya uzembe kutona na uvimbe wa tumbo ambao alikuwa nao baada ya kuugua kwa muda,kitu ambacho kilitokea madaktari walimfanyia upasuaji bila kufanya uchunguzi.
“na ikashindika kumrudisha katika hali yake ya kawaida kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na kansa ambapo akuchua muda akafariki dunia na timu yetu ya reli ya morogoro ikakosa kipa ambaye akikuwa akicheza kwa kiwango cha juu sana kipindi, hicho mungu amlaze mahali pema peponi,Ameni.
Imani za kishirikana.
“zilikuwepo,zipo,zitaendelea kuwepo kwa kuwa ushirikina ni imani na wanamichezo wengi wanatumia na wanaamini kuwa zinasaidia mfano ukimwangalia Drogba mara nyingi na wachezaji wengine wakiingia uwanjani wanaanza kutanguliza mguu wa kulia,wengine wanashika  nyasi za uwanja pia kuna mchezaji mwingine anaweza akawa anavaa chupi rangi Fulani tu kwa kuwa siku ambayo alivaa chupi hiyo alifunga, kiukweli katika kabumbu kuna mikasa mingi sana ya imani za kishirikina.
Mechi kali
“nakumbuka mechi kati ya Tukuyu Stars pamoja na yanga ambayo ilipigwa mbeya mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 2-2,huku mimi nikiifungia Tukuyu stars bao moja, mchezo huo naukumbuka kwa kuwa mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa mchezaji na badala yake akamtoa mchezaji mwengine baada ya kugundua amekosea akamrudisha uwanjani na kumtoa mchezaji ambaye alifanya kosa, uwanja ukazizima kwa kuwa lilikuwa ni tukio la pekee ninavyofahamu mimi mchezaji akitolewa nje hata kama kwa makosa adhabu inabaki kwa mwamzi.
Baadhi ya nyota waTukuyu stars ni pamoja na  Juma Ahmed, Shaban Katoto, Jimmy Morred, Joshua Kilale, Mohamed Kassanda, Mzee Abdalah, Asanga Aswile pamoja na Raphael Mapunda wengine ni Abuu Ngereza, Sekilojo Chambua,Kanza Mrisho (marehemu) John Mosses, bila kumsahau Salum Kussi nay eye mwenyewe Juma Mtwange Rajabu.
Tofauti ya soka la zamani na sasa.
“zamani sisi tulikuwa tukicheza kwa kutumia vipaji vyetu,na wachezaji wote ambao walikuwa wakicheza mpira walikuwa wakijituma sana,tofauti na sasa ambapo wachezaji wengine hata kama hawana vipaji wanaweza wakakomaa kwa kuwa pesa ipo.
Waamuzi wa Tanzania
“wengi wao ni wabovu ndio maana hawapewi nafsi katika michuano ya kimataifa hilo ni Tatizo kubwa,Waamuzi wetu hawajitambui wanapenda sana rushwa wabadilike ili waweze kufanya vizuri.
Mchezaji nyota
“mbwana Samatta ambaye anakipiga na timu ya Tp mazembe ya nchini kongo nampenda ,ni mchezaji ambaye anatumi akili nyingi akiwa uwanjani na anajituma sana.
Bao kali
“nakumbuka nikiwa tukuyu Stars tulicheza na timu ya Priziner Fc na kipa wa timu hiyo alikuwa amezoea kucheza mpira langoni kwake,mimi nikamwai na kuudokoa na kufunga bao zuri,na wachezaji wezake walimlaumu sana kwa tukio lile.
Soka la Iringa.
“kicha changu kinauma sana kuhusu soka la Iringa,kama ningepewa nafsi ya kutoa ushauri na watu wote kunisikiliza ningeshauri kuwa iazishwe timu mpya ambayo itawaunganisha wanairinga wote na itumie jina la Iringa city jina ambalo litapendwa na wanairinga wote kama ilivyo mbeya city huko mbeya.
“vile vile mkoani  Iringa kuna mpasuko mkubwa sana, mfano watu wengi wanaichukia lipuli kwa kuwa ni timu ambayo inasadikika ni moja ya tawi la timu kubwa toka Jijini Dar,ambapo kuna baadhi ya mashabiki wa timu hizo za dar lazima wataionea gere.
Mwisho wa soka  
Nina mke na watoto 6,umri wangu ni miaka 44,nipo jijini Dar najishughurisha na biashara zangu ambazo zinaniwezesha kuishi vizuri na familia yangu.


Chapisha Maoni