Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Sophia Mwaipyana,Mbeya


Timu ya Mbeya City  ya jijini hapa  inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho  na Timu ya Vipers kutoka Uganda katika Uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Ikiwa ni moja ya maandalizi ya ligi kuu inayotalajia kuanza kutimua vumbi  hivi karibuni .
Akiongea na jelambaviwanjani ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten  alisema  kwamba mchezo huo wa kimataifa  nikwajili ya kujipima  baada ya kufanya mazoezi ya kujiandaa kwa ligi kuu ya bara.
 
Ten alisema Timu ya Viper inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Uganda na kwamba msimu uliopita ilishika nafasi ya nne kati ya timu 12.
 
Alisema timu hiyo ilitarajiwa kuwasili jijiji hapa leo jioni kwa ndege ya Fast Jet na kwamba waliondoka Uganda Saa 4.00 asubuhi ya leo.
 
Alisema kiingilio cha mechi hiyo kitakuwa Sh3,000 kiasi ambacho kitawafanya mashabiki wengi wa soka kuingia.
mwisho


Chapisha Maoni