Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
 
Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Prisons Devid Mwamwaja atamani kukipima kikosi chake kwa kupata mechi na timu ya Mbeya City kabla ya ligi kuu kuanza kutimua vumbi.
 
 
Akiongea na MWANDISHI  WETU, Mwamwaja alisema kuwa  natamani sana kama ningepata mechi moja na timu ya Mbeya City  kabla ya ligi kuanza ilikuweza kukipima kikosi changu.
 
“Kwamda uliyo bakia naitaji mechi tatu  kubwa ilikuweza kukamilisha  maandalizi kwajili ya ligi kuu kwani mpaka sasa  maandalizi  yanaendelea vizuri nawachezaji wote wanaendelea vizuri”
 
“Timu imecheza mechi nyingi zakirafiki na juzi tulikuwa mkoani Rukwa tukacheza mechi mbili na zote tumeshinda ila ningefurahi kama ningepata mechi na timu ya Mbeya city lakini mpaka sasa  nazani haita wezekana kwani jumamaosi tunamechi nakimondo Sc  na jumatatu tunaelekea  jijini Dar es salaam”
 
Timu hiyo ambayo inatarajia kuondoka mkoani hapa jumatatu ijayo kuelekea jijini Dar es salaam ambako wataweka kambi huko hadi ligi itakapoanza kwani  mechi yao ya kwanza  wanaanzia ugenini huko mkoani pwani.
 
Mwisho


Chapisha Maoni