Na Alex
Mapunda,Iringa
KUELEKEA
uchaguzi wa viongozi wapya katika timu ya soka ya Lipuli mkoani Iringa Tayari
kamati ya uchaguzi imeshachuja majina ya wagombea na yameshabandikwa katika
mbao za matangazo.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI
mwenyekiti wa uchaguzi wa timu hiyo Jackson Ibrahim Chaula alisema
kati ya wagombea 9 ambao waligombea
katika nafsi mbali mbali jina ambalo ilienguliwa ni la Daudi masasi baada ya kutokidhi vigezo
ikiwemo kukosa cheti cha kidato cha nne pia aliwakata wagombea kuanza kampeni
siku tatu kabla kama zisemavyo kanuni na taratibu za timu hiyo.
“uchaguzi ni
tarehe 28,maandalizi yanaendelea vizuri kikubwa ni kila mgombea kutii taratibu
na kanuni za uchaguzi,ambapo kampeni ni siku tatu kabla ya uchaguzi ambaye
atakiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi
yake”alisema chaula.
Chaula
aliongeza kuwa wanachama wa Lipuli wanatakiwa kujitokeza kwa wingi wakiwa na kadi zao ili kumchagua kiongozi
ambaye ataiongoza timu hiyo kwa ufanisi mkubwa
na ikumbukwe kuwa makosa
watakayofanyika yatawaghalimu wanairinga kwa miaka 4.
Awali
uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika tarehe 28 mwenzi wa nane lakini
wasimamizi waliamua kuahirisha kwa kuwa maandalizi hayakukamirika kwa wakati na
mwenzi huu wamejipanga vilivyo ili kuhakikisha uchaguzi huo unakamirika kwa
kuwapata viongozi wenye sifa.
Chapisha Maoni