Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kuwasilisha rasimu ya Katiba waliyoipitisha, kwa kuzingatia kuwa Muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu wao wa Juni 1 mwaka huu umeainisha baadhi ya marekebisho waliyofanya kwa tulivyowaelekeza.
Yanga wanatakiwa kuwasilisha rasimu hiyo kabla ya Oktoba 5 mwaka huu. Ikiwa itakubaliwa na TFF, itapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo ili waweze kufanya uchaguzi wa viongozi wao.

Kwa upande mwingine
KATIBU Mkuu wa Coastal Union, Kassim
El Siagi atafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kwa kushinikiza mkutano wa wanachama wa klabu hiyo ufanyike bila
kuandaliwa na Kamati ya Utendaji.
Pia El Siagi alitumia vyombo vya habari kuishambulia TFF ambayo haikutambua uamuzi wa mkutano huo ulioelezwa kumdumaza Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Steven Mnguto.
TFF ilimtuma Mkurugenzi wake Msaidizi wa Sheria na Uanachama kufanya uchunguzi wa mgogoro uliokuwa unaendelea katika klabu hiyo.

Baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi huo, TFF imebaini kuwa Mwenyekiti na Mweka Hazina wa klabu hiyo walishajiuzulu, hivyo uitishwe uchaguzi haraka na kujaza nafasi hizo na nyingine zilizo wazi.
Pia wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Salim Amir na Albert Peter wameonywa kwa kushiriki katika mkutano ambao wanajua haukuandaliwa na Kamati ya Utendaji.
Vilevile uchunguzi wa TFF umebaini kuwa ushiriki wa Salim Bawazir na Akida Machai kwenye vikao vya Kamati ya Utendaji ya Coastal Union si halali kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wanachaguliwa na Mkutano Mkuu na si kuteuliwa na Mwenyekiti.
Kwa vile kutakuwa na uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo zipo wazi, uchaguzi huo utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Coastal Union kwa kushirikiana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga na Coastal Union watafanya uhakiki wa reja ya wanachama.
Chapisha Maoni