Kikosi cha Young Africans Sports Club
YANGA
KUIFUATA MTIBWA KESHO
Washindi wa Ngao ya Jamii msimu wa
2014/2015 timu ya Young Africans kesho asubuhi wanatarajia kuondoka jijini Dar
es salaam kuelekea mjini Morogoro tayari kwa mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar katika dimba la Uwanja
Jamhuri.
Kikosi cha Young Africans kimekua
kikiendelea na mazoezi kila siku tangu tangu baada ya mchezo wa jumapili,
ambapo kocha mkuu Marcio Maximo amekua akiwanoa vijana wake kuhakikisha wanakua
fit kwa mchezo huo wa jumamosi.
Young Africans chini ya mbrazil
Marcio Maximo imepania kuhakaikisha safari hii inavunja mwiko wa kukosa ushindi
katika dimba la Jamhuri kwa takribani miaka minne mfululizo, na maandalizi ya
mchezo yanakwenda vizuri kuhakikisha kikosi kinaibuka na pointi tatu muhimu.
Kocha Mkuu Marcio Maximo mara baada
ya mazoezi ya leo katika shule ya Sekondari Loyola, amesema vijana wake wote
fit kwa mchezo huo na kikosi kinatarajia kuondoka asubuhi ili vijana waweze
kupata muda mzuri wa kupumzika.
Aidha Maximo amesema anatambua
Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja kwa muda mrefu, baadhi
ya wachezaji aliwahi kuwafundisha akiwa kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars)
ikiwa ni pamoja na kocha wao Mecky Mexime.
"Sisi tumejiandaa
kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wa jumamosi, natambua utakua ni
mgumu sababu Mtibwa watakua nyumbani wakihitaji pointi tatu muhimu lakini hata
sisi tunakwenda Morogoro kuhakikisha tunapata pointi tatu pia "alisema
Maximo.
Kuhusu maendeleo ya mchezaji Andrey
Coutinho na Jerson Tegete wanaendelea vizuri na mazoezi lakini daktari ameona
wabakie jijini Dar es salaam wakiendelea na programu nyingine chini ya
usimamizi wa madaktari na wataungana na kikosi kitakaporejea jijini kwa mazoezi
ya pamoja.
Wachezaji wanaotarajia kusafiri
kesho kuelekea Morogoro ni:
Makipa: Deo Munishi "Dida", Juma Kaseja na Ally Mustafa
"Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na
Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan Dilunga, Nizar Khalfani,
Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis Kizza, Geilson Santos
"Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa
Last
Updated ( Thursday, 18 September 2014 13:01 )
Chapisha Maoni