John Alex Lwena
John Alex Lwena ni miongoni mwa
wachezaji ambao walikuwa na kipaji cha pekee kuwai kutokea hapa nchini,ambapo
kwa umaili mkubwa alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote kumi na 11 uwanjani na
kucheza juu ya kiwango.
Alex mzaliwa wa Namatui huko
Mpitimbi Songea Vijijini alianza kusakata kabumbu katika shule ya msingi
Mpitimbi ambapo baada ya kumaliza shule ya msingi akatimukia kwa kaka yake
ubaruku mbeya ambako alijiunga na timu ya Rubiga Fc huko Tukuyu.
Katika mazungumzo maalum na gazeti
hili nafafanua zaidi kuhusu maisha yake ya soka;
“Nilianza kucheza soka la ushindani nikiwa na Tukuyu Stars timu ambayo iliundwa
kwa mara ya kwanza na wachezaji wengi toka Rubiga Fc wakati huo ilikuwa
ikifahamika kwa jina la Limbe Kabla ya Tukuyu Stars timu ambayo tuliipandisha
Moja kwa moja Toka madaraja ya chini na kufanikiwa kuchukua ubingwa mwaka 1986.
“Na baada ya uwezo wangu kuwa katika
kiwango cha juu Mwaka 1989 yanga wakanichukua kipindi ambacho nilipata nafsi ya
kuchezea timu ya taifa kuanzia mwaka 1989-1990 ambapo mwaka 1994 niliondoka
yanga na kujiunga na timu ya Maji Maji ya songea kwa ubadhirifu wa
usajili ambao sita kuja kuusahau hadi nitakapoingia kaburini ambao ulifanywa na
aliyekuwa kiongizi wa yanga bwana Mpondela.
“kilichotokea Yanga walituacha
katika kikosi hicho dakika za mwisho na majina yetu wakawaingiza wachezaji toka
nje hali ambayo iliniuma sana kwa kuwa hadi siku ya mwisho ya usajili majina
yetu tuliyahakiki na yalikuwepo.
“Na baada ya muda wa usajili kuisha
habari zikatoka kwenye magazeti kuhsu usajiri cha kusikitisha majina yetu
hayakuwepo hali ambayo ilitufanya tuishiwe nguvu ambapo kwa kipindi kile
ilikuwa ukiachwa kwenye usajili ililazimika kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
“Hayo yote yalitokea baada ya
kubadilika kwa uongozi ndani ya Yanga ambapo viongozi wapya walikuja na
falsafa ya kuwapandisha vijana wengi toka kikosi B na kutuacha wachezaji wengi
ambao tulikuwa wakongwe na wazoefu katika timu ile.
“Hali mabayo ilizua mtafaruku mkubwa
sana kati ya viongozi na wanachama ambao walioji kwa nini wametufanyia kitendo
cha kinyama dakika za mwisho,viongozi wakakosa jibu na wakakili wamekosea
baadae suala lile wakalifikisha TFF ili sisi tuingizwe kwenye usajili lakini
kwa bahati mbaya Tff walikataa kwa kuwa taarifa tayari zilikuwa zimishatoka
kwenye vyombo vya habari.
“Hatukuwa na jinsi lakini kitu
ambacho kilitokea baada ya sisi kuachwa katika kikosi kile Yanga walinusurika
kushuka daraja kutokana na kwamba walikuwa na kikosi dhaifu sana kikosi ambapo
kilipoteza mechi nyingi sana katika ligi.
“Nashukuru Mungu baada ya tukio lile
sikukaa sana nje ya uwanja Maji Maji wakanichukua bila kuchelewa hawali
wakaniingiza kwenye kikosi cha timu ya Mkoa wa Ruvuma na baadae
wakinisajili moja kwa moja Timu ambayo niliitumikia hadi mwaka 2002 kwa
mafanikio makubwa sana na baadae nikaachana na soka nikiwa na timu hiyo
na kugeukia shughuli zangu za kawaida,anaeleza Alex kasha anaendelea;
Dini ilimzuia kwenda Oman.
“Wakati nipo yanga kuna kipindi
nilikosa Nafsi ya kwenda kucheza Oman katika ligi ya Mafuta ligi ambayo
matajiri wa oman walikuwa wakikusanya wachezaji wazuri toka Afrika na kwenda
kuunda vikosi vyao na walikuwa wanawalipa pesa ndefu sana.
“Lakini kutokana na kwamba mimi
nilikuwa sio Mwislamu Nikakosa Fursa ya kwenda, mara baada ya kubaini jina
langu lilikuwa sio la kiisilamu na wezangu walipatanafsi ya kwenda kwa kweli
niliumia sana na sikuwa na jinsi kwa kuwa haikuwa bahati yangu.
Hawezi kusahau
“wakati nipo Yanga katika mechi ya
pambano la watani wa Jadi Simba na Yanga nakumbuka niliumizwa Goti kwa Makusudi
na mchezaji wa Simba Omari Mavisu kwa kuwa nilikuwa nampelekesha sana ali
ambayo ilinilazimu kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na katika mechi ile
Simba walipata ushindi wa bao 1-0.
“kitu Ambacho sita kuja
kukisahau baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miezi miwili kulikuwepo na mechi
kali sana kati ya Yanga na Coastal Union ya Tanga wataalamu wa nje ya uwanja wa
Yanga wakasema kwenye mechi ile mimi lazima nikacheze na wakasema wachazaji
wengine wote nyota zao zilikuwa zimefutika na nyota pekee ambayo ilikuwa
inang’aa ni nyota yangu.
“kwa kipindi hicho nilikuwa hata kutembea
siwezi lakini mtaalam mmoja akanichanjia dawa kwenye goti kabla ya mechi na
wakanitaka kuingia mchezoni dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika ili kugusa
mpira na kuziweka sawa nyota za wezangu.
“Na mechi ile yanga waliichukulia
kwa uzito mkubwa kwa kuwa kama tungefungwa au kutoa sare Tungetolewa kwenye
mbio za kuuania ubingwa mwaka 1990 kweli dakika 20 kabla ya mtanange kumalizika
wakaninyanyua kwenye benchi na kuingia uwanjani.
“uwezi kuamini kitu ambacho
kilitokea kwa mara ya kwanza nilikuwa natembea vizuri na nikawa na uwezo wa
kukimbia uwanjani,mara baada ya kuingia uwanjani na mimi kugusa mpira
hazikupita dakika tano tukapata bao ambalo lilifungwa na Keneth Mkapa bao
ambalo lilidumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Ushirikina Michezoni
“unafanywa sana na nchi zote za
kaafrika,kila mtu na imani yake lakini kwa viongozi wa timu hadi hivi sasa hayo
mambo yapo na bado yanaendelea.
“Nakumbuka wakati nikicheza wakati
mwingine ilikuwa inatulazimu kuruka geiti au kuruka ukuta kwa kutumia ngazi kwa
imani za ushirikina mambao ambayo yanafanywa sana hasa na Timu kubwa
Simba na Yanga.
Mechi anayokumbuka
“Naikumbuka Sana Mechi yangu ya
kwanza ya kimataifa kati ya Tukuyu Stars na Sports club Villa katika
michuano ya afrika mashariki na kati sisi tukiwa wawakirishi wa nchi,
Mechi ambayo ilikuwa ngumu na Villa
wakaibuka na ushindi wa bao 4-0.
“siwezi kuisahau mechi ile kwa kuwa
wachezaji wengi ambao tulikuwa tukichezea tukuyu stars ilikuwa mechi yetu ya
kwanza ya kimataifa licha ya kwamba tulicheza vizuri katika mchezo ule lakini
Villa wakatutundika bao nne kutokana na uzoefu wao katika mashindano ya
kimataifa.
Mchezaji anayemkubari
.
“Niyozima ananikosha sana ni moja ya
viungo bora tulionao katika ligi ya hapa nyumbani ambapo tunaweza kufananisha
na viungo wa zamani wa hapa nchini.
Namba zote uwanjani zilikuwa mali
yake
“Nlilikuwa na uwezo wa kucheza namba
zote nikiwa uwanjani na nilikuwa na nguvu na uwezo nkubwa wa kukimbia na mara
nyingi nilikuwa napangwa nafasi ya winga kwa kuwa nilikuwa na uwezo wa kupiga
mashuti kwa kutumia miguu yote miwili kama Ronaldo,na nilikuwa jasiri kutokana
na mazoezi magumu ambayo nilikuwa nikiyafanya.
“kwa mabeki ambao waliwai kukutana
na mimi awawezi kunisahau katika maisha yao kwa kuwa mbinu zote za beki nlikuwa
nazifahamu na nilikuwa nakiwaumiza vichwa.
“Kuna kipindi wakati nipo Tukuyu
Stars wakati tunapigania kupanda Daraja katika ligi ya kanda mlinda mlango wetu
alikuwa ameumia mimi nikachukua jukumu la kusimama golini,kwa kweli nilicheza
kwa umahili mkubwa sana na kutokana na uwezo wangu kuwa nzuri sikuruhusu bao
lolote siku ile, ambapo tuliibuka na ushindi wa bao 3-0.
Nidhamu
“Nidhamu ndio kila kitu katika mpira
mimi nakumbuka pindi nacheza sikuwai gombana na viongozi au wachezaji wezangu
kwa kuwa nilikuwa na nidhamu lakini viongozi wa timu mara nyingi wanatumia
nidhamu vibaya kwa wachezaji hasa wakati wa usajiri kama kuna pesa ulikuwa
unawadai ikifikia wakati wa usajili ukiwadai wanatishia kukutema ambapo mara
nyingi wachezaji wengi wanapoteza sana pesa zao wakati wa usajili.
“Lakini kuna baadhi ya wachezaji
toka wakati wa enzi zetu hawakuwa na nidhamu lakini walikuwa na uwezo wa hali
ya juu sana mfano Saidi mwamba wakati tunacheza nae alikuwa mlevi wa
kupindukia, nakumbua alikuwa anatoroka kambini kwenda baa na kuletwa akiwa
amebebwa na kuna wakati mwingine alikuwa anawatukana adi viongozi wa club.
“lakini alikuwa na uwezo wa hali ya
juu sana kiasi kwamba licha ya nidhamu yake kuwa mbovu lakini akikosekana yeye
uwanjani ilikuwa ngumu sana kupata ushindi tofauti na wachezaji wa sasa wengi
wao hawana nidhamu lakini kucheza mpira hawajui.
Baada ya kustaafu
Sasa ninafanya kazi Tanesco
kabla ya hapo nilikuwepo Sido nikifanya kazi ya kuchomelea vyuma,nashukuru
mungu maisha yangu yanaenda vizuri ingwa soka sikunufaika nalo chochote
kiuchumi zaidi ya kunionyesha dira ya maisha kwa kufamaniana na watu wengi.
“kwa sasa nina miaka 43 hadi 2013
naishi Songea,nina mke na watoto wanne.anahitimisha John Alex Lwena.
Chapisha Maoni