Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na A lex Mapunda,Iringa
JUMLA ya wachezaji 37 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya copa coca cola mkoa wa Iringa ambapo kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini leo siku ya Jumatatu mkoani hapa.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI  Katibu wa chama cha Soka mkoa John Mwakarobo alisema wachezaji hao wamewachukua toka kila Wilaya kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa katika michuano hiyo,pia wakiwa kambini watafanyiwa mchujo hadi kufikia wachezaji 25.
“wachezaji hao tumewapata toka kwenye mashindano ya copa cocacola wilaya kupita kwa walimu ambao tuliwapa kazi ya kuwachuja wachezaji hao , mkoa wa Iringa baada ya kujigawa una wilaya nne,wilaya ya kilolo,Mfindi,Iringa vijijijni pamoja na Iringa Mjini ambapo wilaya zote zimetoa wachezaji wazuri.
“tumewapata vijana wenye vipaji hivyo tunaamini  watafanya vizuri katika mchezo wa kwanza dhidi ya vijana wa mbeya  mchezo ambao utafanyika tarehe 12,mwezi huu pamoja na michezo mingine”alisema mwakarobo.
Michuano ya kopa coca cola inafanyika kila mwaka kwa hapa nchini ikiwa na lengo la kuendeleza soka toka kwa vijana wadogo, ambao watakuja kuwa tegemeo  hapa nchini kwa miaka ya baadae.


Chapisha Maoni