Mkutano Mkuu wa Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam
ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye
bodi hiyo.
Nafasi hiyo ya ujumbe
kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa ikishikiliwa na Kazimoto Muzo
imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba ya Mwanza kushuka daraja kutoka la
Kwanza hadi la Pili.
Hivyo, wagombea wa nafasi
hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Klabu hizo zina
nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB ambapo nyingine inashikiliwa
na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya Shinyanga.
Chapisha Maoni