YANGA Vs JKT RUVU JUMAPILI
F
Baada ya kupata ushindi wa kwanza wa mabao 2-1 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza Tanzania Prisons, timu ya Young Africans itashuka tena dimbani siku ya jumapili[LEO] kucheza na maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa (Ruvu JKT Stars) kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha mbrazil Marcio Maximo kimeingia kambini jana jioni katika Hoteli ya Valley View kikiwa na wachezaji 26 kujiandaa na mchezo huo wa siku ya jumapili ambao utakua ni mchezo wa tatu katika ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Young Africans ambayo inashika nafasi ya nane kati ya timu 14 zilizopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi tatu, inahitaji kupata pointi tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusogea katika nafasi za juu kwenye msimamo.
Kocha Marcio Maximo amesema vijana wake wamekua wakifanya mazoezi kila siku katika Uwanja wa shule ya sekondari Loyola kujiandaa na mchezo huo ambao anasema utakua ni mgumu kutokana na maafande wa JKT kuingia uwanjani kusaka ushindi wake wa kwanza.
"Nimewandaa vijana kufanya vizuri kwenye mchezo unaofuata, makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya timu ya Tanzania Prisons tumeyafanyia kazi na naamini wachezaji wameelewa nini wanapaswa kukifanya uwanjani siku ya jumapili alisema" Maximo.
Habari njema ni kurejea dimbani kwa mshambuliaji Hussein Javu na mlinzi wa kushoto Oscar Joshua ambao walikuwa majeruhi, kwa sasa afya zao ziko safi na wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine kujiweka fit kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu.
Aidha kocha Marcio Maximo amesema kwa sasa kikosi chake kwa sasa hakina majeruhi hata mmoja, wachezaji wote 32 wako salama kiafya, fikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo na kuwaomba wapenzi, wanachama na washabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani siku ya jumapili kuja kuishangili timu yao.

MECHI ZA LEO
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Mtibwa Sugar Vs Mgambo
MATOKEO YA JANA
Simba SC 1-1 Stand Utd
Coastal 2-1 Ndanda FC
Polisi 1-1 Kagera Sugar
Prisons 0-0 Azam FC
Ruvu Shoot 0-0 Mbeya City
Chapisha Maoni