Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Simba wapata ushindi wa kwanza Iringa
Na Alex Mapunda,Iringa

Baaada ya kuambulia sare mfurulizo katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wekundu wa msimbazi Simba wameosha nyota yao kwa kuitandika Lipuli ya Iringa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa samora mkoani Iringa.
Katika mchezo huo ambao Lipuli walicheza vizuri kuliko mechi zao zote ambazo wamewa kucheza msimu huu katika ligi daraja la kwanza,  hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipokati timu hizo zilienda mapumziko milango yote ikiwa imenuna.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mbwembwe na kasi kubwa huku kila timu ikiwa na uchu wa kutaka kuibuka na ushindi,huku wakishuudiwa na mashabiki rukuki toka kona mbali mbali za mkoani iringa alikuwa ni Elius Maguri aliyewainua mashaki wa Simba kwa kufunga bao safi ambalo lilikwamishwa kimiani kwa umaili mkubwa Dakika ya 54 ya mchezo bao ambalo lilidumu hadi dakika ya mwisho ya mwamuzi.
Baada ya mchezo huo Katibu msaidizi wa Lipuli Ronjino Malambo aliwapongeza wachezaji wa Lipuli kwa kucheza vizuri katika mchezo huo na kuwataka kuamishia makali hayo katika mchezo dhidi ya Kimondo Fc toka Mbozi mbeya unaotarajiwa kuchezwa wikendi hii.
Simba wanatarajia kuvaana na mtibwa Sugar wikendi hii mkoani Morogoro ambapo ikumbukwe kuwa hadi kufika hivi sasa mtibwa  anaongoza ligi kwa kufikisha pointi 13 wakifuatiwa na Azam fc wenye pointi 10 huku Simba wakikamata nafsi ya 9 kwa kufikisha pointi tano baada ya kuambulia pointi moja moja katika michi zao zote za ligi hiyo.


Chapisha Maoni