shirikisho la soka la afrika caf
limeichagua na kuipatia nafasi guinea ya ikweta kuandaa fainali za kombe la afrika
2015 kuchukua nafasi ya moroko iliyojitoa wiki iliyopita. awali rais wa caf
issa hayatou alikuwa na majadiliano yenye manufaa na rais wa nchi hiyo tajiri
ya mafuta teodoro obiang nguema mjini malabo kabla ya kufikia hatua ya
kuikabidhi nchi yake dhamana hiyo.
taarifa ya caf imethibitisha leo
ijumaa kuwa guinea ya ikweta mojawapo ya nchi ndogo barani afrika imepewa
jukumu hilo kubwa la kuokoa jahazi la michuano hiyo na itashiriki fainali hizo
kama ilivyo kawaida ya mwenyeji.
nchi hiyo yenye kutumia kihispaniola
kama lugha ya taifa iliandaa fainali za afrika za mwaka 2012 kwa pamoja na
jirani yake gabon. mashindano hayo yatafanyika kuanzia januari 17- februari 8
mwakani kwenye miji ya bata, ebebiyin, mongomo na mji mkuu malabo. mwaka 2012
walitumia miji miwili tu ya bata na malabo.
ratiba kupangwa malabo
sherehe za kupanga ratiba ya mechi
za fainali hizo itafanyika mji mkuu wa malabo mnamo desemba 3 mwaka huu.
taarifa ya caf imesema kuwa shirikisho hilo linawashukuru watu wa guinea ya
ikweta, serikali pamoja na rais ngwema mwenyewe kwa utayari wao wa kuokoa
mashindano hayo. moroko ilijitoa kaandaa fainali hizo baada ya kuomba caf
isogeze mbele mashindano kwa ajili ya hofu ya ugonjwa wa ebola ambao umeenea
kwenye nchi kadhaa za afrika magharibi ambazo kwa kawaida hupeleka timu nyingi
zaidi katika fainali za afrika.
caf ilikataa mpango huo kwa madai
kuwa haijawahi kuahirisha wala kufuta fainali hizo tangu kuanzishwa kwake mwaka
1957. moroko walipewa hadi jumamosi iliyopita kuthibitisha utayari wao wa
kuandaa mashindano hayo lakini walishindwa kufanya hivyo na caf ikaamua kufanya
mchakato wa kutafuta nchi ya kuokoa na hatimaye imepatikana hii leo.
shirikisho hilo limeipa adhabu
moroko ya kutoshiriki fainali zijazo za huko guinea ya ikweta.
BBC
Chapisha Maoni