Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





NA Alex Mapunda,Iringa




Timu ya Lipuli mkoani Iringa Imevutwa sharti katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare na Tessema Fc,katika mchezo wali ligi daraja la kwanza uliofanyika katika uwanja wa samora mkoani Iringa.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa na mashambulizi mengi, kila timu itabidi ijilaumu kwa kukosa nafsi za wazi ambapo hali hiyo ikadumu hadi dakika 90 za mchezo na kila timu ikatoka uwanjani mikono kichwani.


Timu ya lipuli kwa sasa inatakiwa kucheza kwa kujituma zaidi ili kuhakikisha inapanda daraja mara baada ya kucheza madaraja ya chini kwa muda mrefu bila mafanikio.


Kwa upande mwingine timu ya Kurugenzi ya mafinga nayo imetoka sare dhidi ya Kimondo Fc katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa mvuwa wilayani Mbozi mbeya.




Chapisha Maoni