Kocha wa simba Patrick Phiri akiwa na wachezaji wake, wakipasha katika uwanja wa samora.
LICHA ya uwanja
wa Samora kuwa uwanja wa michezo na burudani,Kaimu katibu mkuu wa chama cha
soka mkoa wa Iringa John Mwakarobo amewatakaa wameriki wa uwanja huo kuzuia
baadhi ya shurughuli za burudani kufanyika katika uwanja huo ili kurinda na
kutuza miundombinu ya uwanja huo.
Akizungumza na Jelamba viwanjani mwakarobo alisema,miundombinu
ya uwanja wa Samora inazidi kuwa hatarini ikiwemo pichi ya
kuchezea kutokana na shughuli za kiburudani na zingine za kijamii zinazopelekea
kujaza watu wengi huwanjani hapo.
“kuna baadhi ya shughuri kama Fiesta pamoja na Mtikisiko ni
shughuli ambazo zinazalisha uchafu mwingi katika uwanja wa samora,pia shughuli
ambazo zinasababisha kuwepo kwa mashomo katikati ya uwanja,nawaomba wamiriki wa
uwanja huo kufanya maamuzi mazuri ambayo yatapelekea kuinusuru hali ya uwanja
wa samora.
Pia mwakarobo aliongongeza kuwa wamiriki wa uwanja huo wanatakiwa
kushirikiana bega kwa bega na uongozi wa chama cha soka pamoja na wadau wa
michezo mkoani hapa ili kuhakikisha wanatatua matatizo sugu ya uwanja huo
ikiwemo,tatizo la uzio,pichi ya kuchezea pamoja na mapungufu mengine yote ya
uwanja huo ambapo kama Lipuli watapanda daraja msimu ujao wawe na sehemu zuri
ya kuchezea.
Lipuli ambayo inatumia uwanja wa Samora kama uwanja wake wa
nyumbani wmemaliza katika nafsi ya tatu mzunguko wa kwanza ligi daraja la kwanza ambapo kama watafanya vizuri mzunguko
wa pili wananafasi kubwa ya kupanda daraja msimu huu.
Chapisha Maoni