Bendera
zinapepea nusu mlingoti katika viwanja vya cricket nchini Australia
katika kuomboleza kifo cha mcheza crickte Philip Hughes aliyefariki hapo
jana baada ya kupigwa na mpira. Salaam za rambi rambi zimeendelea
kutolewa kutoka sehemu mbali mbali duniani. Baadhi ya wachazaji wa
cricket wamekuwa wakiacha magongo ya mchezo huo katika mlangoni mwa
nyumba zao kama ishara ya kuomboleza kifo hicho.
Naye mwanasoka wa maarufu wa
zamani Edison Arantes do Nascimento almaarufu Pele amesema anaendelea
vizuri baada ya kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na
kusumbuliwa na tatizo la njia ya mkojo.Taarifa zinasema Pele alipelekwa hosptalini hapo na kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Na kindumbwembwe cha ligi kuu ya England kinaendelea kesho ambapo Arsenal watasafiri kumenyana na West Bromwich Albion huku Manchester United wakipepetana na Hull City Mechi ambayo itatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC kuanzia majira ya saa kumi na moja kwa saa za Afrika Mashariki. Mechi nyingine Sunderland wataumana vikali na Chelsea na Liverpool wakikutana uso kwa uso na Stoke City.
..Ndondi za kulipwa za shirikisho la kimataifa, Aiba, zinaendelea wikendi hii nchini Argentina na Azerbaijan, huku klabu ya Twende ya Tanzania, ikizidi kupata kichapo kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika ya mchezo wa magongo mjini Bulawayo, Zimbabwe
by http://www.bbc.co.uk
Chapisha Maoni