Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




 
MCHEZAJI  wa zamani  wa timu ya Brazil Ronaldo  alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tenisi Rafael Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha zote.

Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.
 BY BBC


Chapisha Maoni