Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




  Sitti Abbas Mtemvu ametamka rasmi kuvua taji hilo ambalo alilitwaa 0ktoba 11 mwaka huu kwenye fainali za shindano zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Katika barua iliyoandikwa na Sitti kwenda kwa Kamati ya Miss Tanzania Sitti alisema  hivi: Sitti Abbas Mtemvu S.L.P 60 151 Dar es Salaam 5.Novemba 2014.

Mkurugenzi Lino International Agency Limited Dar es Salaam, Yah:Kuvua  taji la Miss Tanzania 2014.

Ndugu Mkurugenzi  tafadhali husika  na kichwa cha habari hapo juu, “Mimi Sitti Abbas Mtemvu, baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania mwaka 2014 kumezuka  shutuma  mbalimbali dhidi yangu .Wameniwekea  maneno  mengi sana  mdomoni  kwamba nimesema wakati siyo”.

Shutuma hizo  zimeandikwa  katika vyombo mbalimbali vya habari , Blogs na Mitandao ya Kijamii, kiasi ambacho naona inaweza hata  kuhatarisha  maisha yangu.
Sasa  kwa hiari yangu  mwenyewe tena  bila  kushawishiwa  na mtu  na  kwa kulinda  heshima yangu  pamoja  na familia  yangu  natamka rasmi kuvua  taji la urembo  la Miss Tanzania 2014.



Chapisha Maoni